Vyombo vya habari vya Marekani vyadai makombora ya Iran Yaliitungua Ndege ya Ukraine

Marekani wanaamini Ndege ya Abiria ya Ukraine 'Boeing 737 iliyoanguka Iran na kuua watu 176 ilitunguliwa kwa bahati mbaya na Iran 

Maofisa wa Marekani kwa mujibu wa runinga ya CBS wanasema mitambo ya Satellite imenasa makombora mawili ambayo yalirushwa kabla ya Ndege kuanguka yakifuatiwa na mlipuko mkubwa.

Ukraine awali ilisema kuwa inachunguza endapo ndege yake iliangushwa na kombora, jambo ambalo mamlaka za Iran zilikanusha vikali.

Kuanguka kwa ndege hiyo kulitokea saa chache baada ya Iran kushambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq kwa makombora ya masafa marefu.

Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Alhamisi alisema: "nina mashaka" juu ya (kuanguka) kwa ndege. "Inawezekana kuna mtu amefanya kosa kubwa."

Iran imetangaza kutokabidhi kisanduku cheusi cha kuhifadhi taarifa za ndege kwa kampuni ya ndege ya Boeing ama serikali ya Marekani kwa uchunguzi wa ajali hiyo.

Hatua hiyo inatokana na mzozo uliokomaa baina ya Marekani na Iran

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post