
Ilikuwa
majira ya saa 7:54 usiku akiwa amemaliza kuimba wimbo wa Tetema na
Rayvany, ambapo simu hiyo ilipelekwa jukwaani na Katibu Itikadi na
Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akiongozana na
meneja wake Babu Tale.
Baada
ya kuipokea aliwatangazaia mashabiki waliofika uwanjani hapo kwamba
‘Wanakigoma nimewaambia kitu si nimewaambia leo mna bahati sana, kwenye
simu tuko na Mheshimiwa Magufuli piga shangweeee, Mheshimiwa shikamooo.
Baada
ya hapo akaweka sauti kubwa ambayo ilikuwa ikisikika kwenye spika, na
kumwambia nakutakiwa wewe heri ya mwaka mpya pamoja na Wanakigoma wote,
wakati huo mashabiki wakawa wanapiga kelele za babu!babu!babu!.
Kutokana
na hali hiyo Diamond aliwatuliza, lakini bado hawakusikia na kuendelea
kupiga kelele. Rais amesema alitamani na yeye angekuwepo hapo, lakini
amemtuma Polepole na wengine waliokuja hapo.