Kesi ya Erick Kabendera Yapigwa Kalenda hadi Februari 10

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili, mwandishi wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera, umeieleza Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kuwa, mchakato wa makubaliano kati ya Kabendera na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) bado unaendelea.

Wakili wa Serikali Gloria Mwenda amedai hayo leo Januari 27,2020 Mbele ya Hakimu Mkazi, Jenet Mtega wakati kesi hiyo ilipokuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Mwenda amedai upelelezi bado unaendelea na mchakato wa makubaliano kwa DPP pia unaendelea hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

 Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 10 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173.Kwa mara ya kwanza Kabendera alifikishwa mahakamani hapo Agosti 5, 2019 akikabiliwa na makosa hayo anayodaiwa kuyafanya kati ya Januari 2015 na Julai 2019, jijini Dar es Salaam.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post