KESI YA ERICK KABENDERA YAPIGWA KALENDA HADI JANUARY 27


Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera, umeielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi katika kesi hiyo umebakia katika maeneo machache kukamilika. 


Wakili wa Serikali, Ester Martin ameileleza Mahakamani hiyo jana  Jumatatu, Januari 13, 2020 wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Martin alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Janeth Mtega upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kwamba wanamalizia vitu vichache ili kukamilisha upelelezi wa shauri hilo.

Hakimu Mtega baada ya kueleza hayo, aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 27, 2020 itakapotajwa.
Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kutakatisha fedha kiasi cha Sh173 milioni, katika Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post