
Hata hivyo ilisema hakukua na taarifa mpya za vifo iliyothibitishwa tofauti na jimbo la Hubei, ambako mapema liliarifu watu 24 waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi hivyo wanafanya idadi ya waliokufa hadi sasa kufikia 80.
Rais wa China Xi Jinping ameuita mripuko huo kuwa ni hali ya wasiwasi mkubwa na kusema serikali ilikuwa inafanya juhudi za kuzuia safari na mikusanyiko ya umma wakati ikiwapeleka wahudumu wa afya na vifaa kwenye mji ambao ni kitovu cha janga hilo wa Wuhan.