Iran Yasema Mashambulizi Ya Leo Dhidi Ya Marekani Ni Kama Makofi ya Uso Tu

Kiongozi mkuu wa  Iran, Ayatollah Ali Khamenei amesema hii leo kwamba shambulizi la makombora kwenye kambi za kijeshi zinazotumiwa na Marekani nchini Iraq ni kofi la uso kwa taifa hilo na  amesisitiza hatua hiyo ya kijeshi haitoshi. 

Ayatollah amelihutubia taifa masaa kadhaa baada ya kushambulia kambi hizo za kijeshi.

Shambulizi hili ni la kisasi dhidi ya mauaji ya jenerali wa kikosi maalumu cha Quds cha Iran, Qassemi Soleimani aliyeuliwa na Marekani mjini Baghdad Ijumaa iliyopita. 

Khamenei amesema uwepo usio halali wa Marekani kwenye ukanda huo unatakiwa kumalizwa akisema umesababisha vita, mgawanyiko na uharibifu. 

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohamad Zarif amesema shambulizi hilo ni sawa na hatua za kujilinda huku rais wa halmashauri ya Ulaya Ursula von der Leyen akitoa mwito wa kufanyika makubaliano ya kidiplomasia.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post