AJINYONGA KWA HASIRA BAADA YA MKEWE KUUZA KONDOO NA KUTUMIA FEDHA BILA KUMSHIRIKISHA


Na  Rehema Matowo, Mwananchi 
 Paulo Hassan, mkazi wa kijiji cha Gamash, kata ya Bulela wilayani Geita, anayekadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 40 anadaiwa kujinyonga na shuka kwa kile kinachodaiwa kuwa ni hasira baada ya mkewe kuuza kondoo na kutumia fedha bila kumshirikisha.
Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, mke wa marehemu, Jenipha Lateremla alidai kuwa mumewe alijinyonga usiku wa kuamkia Januari 18,2020 baada ya kutokea ugomvi baina yao.
Jenipha alisema usiku wa Januari 17 wakiwa chumbani, mumewe alianza kuhoji alikopeleka kondoo, alimueleza kuwa alimuuza kwa ajili ya maandalizi ya Sikukuu ya Krismasi na fedha hizo alizitumia kwenye sikukuu.
“Tukiwa tumelala usiku, akaniambia tena, unajua moyo wangu ulivyo na hasira, hela umefanyia nini nilivyoona hivyo kwa kuwa akikasirika huwa ananipiga nilitoka nje nikamuacha,” alisema Jenipha.
Alisema alipotoka nje mumewe alifunga mlango na mkewe akabaki nje na kuwagongea watoto na asubuhi watoto walipoamka walimgongea baba yao kwa ajili ya kumsalimia, lakini hakuitikia na walipochungulia ndani walikuta amejinyonga kwa shuka yake ya kulalia.
Via Mwananchi

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post