JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LASEMA LINAMSHIKILIA TITO MAGOTI KWA MAHOJIANO


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linamshikilia ofisa programu wa kituo cha sheria  na haki za Binadamu (LHRC), Tito  Magoti kwa mahojiano.


"Tunamshikilia Tito Magoti (26), Mkazi wa Ubungo Kibo, Afisa Programu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ( LHRC ) pamoja na Watu wengine watatu kwa uchunguzi na mahojiano kwa tuhuma za makosa ya jinai, Tito hajatekwa ”- Amesema Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Awali, Magoti ilidaiwa kuwa amechukuliwa na watu wasiojulikana leo mchana Ijumaa akiwa kituo cha mafuta cha Puma kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post