IGP Sirro Asaini Mkataba Wa Makubaliano Wa Kuwajengea Uwezo Maofisa Na Askari

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesaini mkataba wa makubaliano wa miaka mitano utakaosaidia katika kuwajengea uwezo maofisa na askari wa Jeshi hilo wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

Akisaini mkataba huo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dodoma IGP Sirro amesema kuwa, wameendelea kushirikiana na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba  Mwekundu ICRC katika kuhakikisha wanaendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa maofisa na askari kuhusiana na masuala ya haki za binadamu.

Kwa upande wake Mkuu wa Misheni Andrea Heath amesema kuwa, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC imeendelea kuwa na ushirikiano mzuri na Jeshi la Polisi nchini na kwamba mkataba huo wa miaka mitano utasaidia katika kufanya mafunzo mbalimbali ikiwemo semina za masuala ya baharini huku lengo likiwa ni kupunguza uhalifu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post