
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad amekanusha taarifa zilizodai kuwa alikuwa ametekwa.
Akizungumza
na Azam TV, Prof Assad amesema siku ambayo inadaiwa alichukuliwa na
watu wasiojulikana, alikuwa kwenye hafla ya kidini wilayani Kisarawe.
""Tangu
juzi nilipewa mwaliko wa siku tatu na watu wa Umoja wa Wanataaluma wa
Kiislamu Tanzania (Tampro) kwenda kwenye warsha Kisarawe kuzungumzia
namna ya kuhuisha taasisi hiyo na niliwaambia nitakuwapo kwa siku moja
badala ya tatu," amesema Profesa Assad
Amesema alimuaga mke wake na kuondoka kwa kutumia gari yake aina ya GD
Wagon mpaka Kisarawe na eneo husika lilikuwa mbali na hakukuwa na
mtandao wa simu wowote unaopatikana.
“Niliingia pale saa 2 tumefanya shughuli ile mpaka nimemaliza kusaliisha
pale saa 3 ndio nikatoka pale na muda nafika Kisarawe mjini simu
zikaanza kuingia lakini mimi nikiendesha gari sipokei simu” amesema
Profesa Assad
Amesema aliendesha hadi kufika maeneo ya Ukonga, Dar es Salaam kwenye
taa za kuongoza magari barabarani kuna kijana wake akampigia simu na
kuipokea.
“Nikamwambia nipo barabarani akasema basi hii inatosha acha niwaambie
nyumbani, nikajua kuna shida nyumbani lakini hakukuwa na shida yoyote
kwangu," amesema ProfesaAssad.
Msikilize hapo chini
Baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof Mussa Assad ametekwa Azam News imezungumza na Prof Assad nyumbani kwake na ameeleza kilichotokea!#AzamNews #AzamTVUpdates #UTV pic.twitter.com/ImWafqpNIJ— Azam TV (@azamtvtz) December 26, 2019