Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 21 Novemba 2019 amefanya
ziara ya kushitukiza ili kujionea hali ya upatikanaji wa mbolea katika
baadhi ya vijiji mkoani Songwe.
Katika
ziara hiyo Mhe Hasunga kadhalika amekagua na kujionea kama
wafanyabiashara wanauza mbolea kutokana na maelekezo ya serikali
iliyopanga bei elekezi na kuitangaza hivi karibuni.
Akiwa
katika ziara hiyo ya kikazi katika kijiji na Kata ya Ipunda katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mhe Hasunga amempongeza mfanyabiashara wa
pembejeo kijijini hapo Ndg Lukas Simkonda kwa kuuza mbolea kwa gharama
ya chini kuliko bei elekezi.
“Wewe
ni miongoni mwa wafanyabiashara tunaowataka, serikali imepanga bei
elekezi lakini wewe umeamua kuuza chini ya bei elekezi ili kuwanufaisha
zaidi wakulima, jambo hili sisi kama serikali tunaliunga mkono na
kukupongeza kwa dhati kwa kazi ya kizalendo unayoifanya” Alisisitiza Mhe
Hasunga
Katika
hatua nyingine Wafanyabiashara wa mbolea nchini wametakiwa kuuza bidhaa
hiyo kwa kufuata bei elekezi zilizotangazwa na Waziri wa Kilimo hivi
karibuni kwani lengo la serikali ni kuhakikisha wakulima wanapata mbolea
ya uhakika na kwa bei nafuu.
Aliitaja
sababu ya kuwa na bei elekezi ya mbolea kuwa ni kukuza kilimo na
kuongeza mavuno ya mazao ambayo ndio malighafi kuu inayohitajika wakati
huu ambapo serikali inatekeleza mipango ya ukuaji wa viwanda, kama
msingi mkuu wa uchumi.
Katika
ziara hiyo Mhe Hasunga akiwa katika zahanati ya Ipunda katika Jimbo
lake la uchaguzi la Vwawa amewapongeza wakazi wa kijiji hicho kwa
kujitokeza kwa wingi kupima Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwani amesema
kupima afya ni msingi wa uimarishaji wa afya zao.
Vilevile
Mhe Hasunga amewataka wakulima kula chakula kizuri chenye mchanganyiko
wa mbogamboga na matunda. “Wakulima wangu mnaniangusha maana ninyi
mnalima na kuzalisha chakula cha kutosha lakini ajabu ninyi ndio
mnaongoza kutokula vizuri jambo hili sio sahihi kabisa, mnapaswa
kuimarisha afya zenu kwa kula vizuri” Alisema Mhe Hasunga
Katika
hatua nyingine Waziri Hasunga amewapongeza wajasiriamali Wilayani Mbozi
kwa kuanzisha viwanda vidogo vya ubanguaji wa karanga kwani vitaongeza
uwezekano wa wakulima kuongeza uzalishaji wa karanga kwakuwai nyenzo za
kubangua zitakuwepo kutokana na teknolojia hiyo ya kisasa.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani
Songwe ameanza ziara ya kikazi ya siku 6 mkoani humo ambapo pamoja na
mambo mengine anakagua hali ya upatikanaji wa mbolea pamoja na kukagua
kama wafanyabiashara wanauza mbolea kutokana na bei elekezi iliyowekwa
na serikali.