;Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika Daniel Urioh.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi
ya wanafunzi wakiwa katika mafunzo ya kubadili Tabia na Uongozi
yaliyofanyika hivi karibuni katika Shule ya Sekondari ya Connerstone
iliyopo Ngaramtoni mkoani Arusha
Wanafunzi
waliohudhuria katika mafunzo ya Kubadili tabia na uongozi yaliyofanyika
katika shule ya Sekondari Connerston wakishangilia baada ya mwenzao
kuonyesha kipaji chake (hayupo pichani)
Wanafunzi
waliohudhuria katika mafunzo ya Kubadili tabia na uongozi yaliyofanyika
katika shule ya Sekondari Connerston wakifuatilia kwa makini kile
kilichokuwa kinaendelea katika Mafunzo
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Ikiwa
leo ni siku ya watoto duniani, jamii imetakiwa kuwajengea uwezo Watoto
kuziishi ndoto zao na kutambua kuwa Watoto huanza Maisha pale
wanapozaliwa hivyo kila hatua iwe wezeshi kwa watoto kufikia ndoto zao.
Limekuwa
ni jambo la kawaida katika jamii kubwa za kiafrika ,wazazi au walezi
kuwalazimisha Watoto wao kufikia ndoto ambazo wao hawajazifikia na haswa
kwa kutumia mifumo rasmi kama ya Elimu ambayo inamuandaa mtoto kuwa
kama jamii inavyotaka na siyo kama apendavyo yeye mwenyewe
‘’Utamsikia mzazi akimlazimisha mtoto wake kwa kumwambia nataka usome uje kuwa daktari,askaripolisi,Mwanajesh i,mwanasheria,mwalimu,bila
kumsikiliza mtoto anapenda kuja kuwa nani ili aweze kumtilia mkazo
Zaidi katika jambo lile alipendalo’’
Daniel Urioh ni
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika amewaambia
waandishi wa habari kuwa wazazi wawe na muda wa kukaa na watoto wao,
wapate kuwasoma, kujua vitu wanavyoelekea kuvipenda waanze kutilia mkazo
,ili waweze kuwakutanisha na watu ambao wamefanikiwa katika sekta hizo,
ili kuwajengea hamasa za kufikia ndoto zao.
‘’
Mazingira ya mtoto huanzia nyumbani pamoja na wale wanaomzunguka,mifumo
sikivu kwa ndoto za watoto siyo kuwafanya waishi kwa matakwa ya kile
wanachokipenda wazazi , jambo ambalo linapelekea mtoto kukwama kufikia
malengo yake pindi anapokuwa mtu mzima na kuanza kujitegemea’’alisema
Mkurugenzi
Ametoa
wito kwa walimu ambao wananafasi kubwa katika Maisha ya Watoto, kuwa
wapo nao muda mwingi Zaidi katika mazingira yao haswa shuleni kuliko mtu
mwingine yeyote, watumie nafasi hiyo kulea ndoto, vipaji, ubunifu
wawatoto hao kwa mbinu zisizodhalilisha,kuumiza au kuwakatisha tamaa
(non-violence strategies)
‘’Baadhi
ya walimu wamekuwa na tabia ya kuua ndoto, vipaji na ubunifu wa Watoto
kwa lugha za kidhalilishaji,za kuumiza na kukatisha tamaa Watoto jambo
ambalo siyo zuri kabisa’’alisema Daniel.
Aidha katika kuadhimisha siku ya Watoto duniani Elimu ya Afrikainachukua
jukumu la kuleta suluhu kwa kutumia programu na makongamano ya kuwatia
moyo, kuwatengenezea majukwaa ya kujifunza na kuonyesha vipaji na bunifu
zao.
Amesema
kuwa Vijana hupata nafasi kushirikiana kwa pamoja, kuhamasishana
kuleta majibu ya changamoto zinazowazunguka na mwisho hutumia vipaji
kuburudisha pia.
Siku
ya watoto duniani huadhimishwa kila mwaka duniani ambapo ilianzishwa
na mwaka 1954 na husheherekewa tarehe 20 mwezi wa novemba kila mwaka
kwaajili ya kuhamasisha na kueneza uelewa miongoni mwa Watoto duniani.



