

Kwandu Mahita akichanganya kemikali katika maabara ya shule ya sekondari Segese.
Mtaalamu wa maabara Esta akiwaelekeza wanafunzi namba ya kufanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari Segese.
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mwalimu wa sayansi katika maabara ya shule ya sekondari Segese jana hayupo pichani.
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mwalimu wa sayansi katika maabara ya shule ya sekondari segese jana hayupo pichani.
Na Salvatory Ntandu - Kahama
Wasichana 91 kati ya wanafunzi 113 wa
jamii za Wafugaji waliohitimu darasa la saba mwaka huu katika shule za
msingi zilizopo katika kata ya Segese katika halmashauri ya Msalala mkoa
wa Shinyanga wameanza kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi ili
kuwahamasisha kupenda masomo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari
mratibu darasa maalumu la elimu kwa wanafunzi wakike, Patrick Mahona
amesema wamejipanga kikamilifu ili kuhakikisha wasichana hao wanapata
haki yao ya msingi ya elimu baada ya kuwanuru wimbi la kuolewa pindi
wanapomaliza elimu ya Msingi.
“Wafugaji katika kata ya Segese mwaka
huu walipiga marufuku tabia za wazazi kuwaoza watoto wao pindi
wanapohitimu darasa la saba kukubaliana kuanzisha darasa maalumu kwa
wasichana 90 ili wajifunze masomo ya awali ya kujiandaa na elimu ya
sekondari”,alisema Mahona.
Mahona amesema katika jamii hizo ndoa
za utotoni zimekuwa zikishamiri pindi watoto wakike wamapohitimu elimu
ya msingi kutokana na wengi wao kutowathamini watoto wa kike hali ambayo
imekuwa ikisababisha kushindwa kupata elimu kutokana na kuolewa hata
kama watakuwa wamefaulu kuendelea na masomo.
Nao baadhi ya Wanafunzi waliopata
mafunzo katika darasa hilo Happness Julius na Kwandu Mashita
wamewapongeza wadau wa elimu katika kata hiyo kwa kutambua umuhimu wa
mtoto wa kike katika masomo hasa kwa kundi la wafugaji.
“Tangu darasa hilo lilipofunguliwa
tumejifunza masomo yote ambayo yatatusaidia kujiandaa na masomo ya
sekondari hapo mwakani ambapo mpaka sasa tumeweza kuingia katika maabara
za sayansi na kujifunza kwa vitendo majaribio mbalimbali",alisema.
Kwa upande Mwalimu Jeconia Mlinda kutoka
shule ya sekondari Segese amesema wanafunzi hao wamejifunza masomo yote
kwa nadharia na vitendo ambayo yatawasidia kufanya vizuri katika masomo
yao hususani ya sayansi.
“Niwaombe wazazi kuwahamsisha watoto
wenu kujifunza masomo ya sayansi kwani yatawasidia kukabiliana na wimbi
la ajira wataalamu wa sayansi wanahitajika sana katika kada mbalimbali
hususani sekta ya afya”,alisema Mlinda.


