WANAODHANI CCM ITANGO’KA MADARAKANI WAMECHELWA-KALLI


NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza,Salum Kalli, amesema CCM wanaodhani itaondoka madarakani wamechelewa bali itaendelea kuongoza nchi kutokana na misingi yake na kukubalika kwa wananchi.

Alisema vipo vyama barani Afrika vilianguka na kuondoka madarakani sababu ya viongozi wake kushindwa kusimamia misingi lakini si kwa CCM.

Kalli alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Bwiru jana kuwa, CCM itendelea kuongoza na kushika kwa miaka 100 kutokana na uimara wa misingi yake na jinsi inavyokubalika kwa wananchi.

“Zipo nchi zinaongozwa kifalme,kidini na kisiasa.Tanzania inaongozwa kisiasa chini ya Chama Cha Mapinduzi , hivyo kitendelea kuongoza kwa muda mrefu kutokana nakutekeleza mmbo mengi ya kijamii, wenye ndoto kuwa kitaondoka madarakaniwamechelewa sana,”alisema.

Katibu wa CCM mkoani humu alisema tangu nchi ipate Uhuru mwaka 1961 ni mengi yamefanywa katika sekta mbalimbali ukiwemo ujenzi wa shule, hospitali, vituo vyaafya na zahanati, reli,miundombinu ya barabara na maji, yote hayo si miujiza nikazi ya CCM.

Alisema wakati nchi inapata Uhuru akina mama walijifungulia vichakani, kulikuwa na shule 22 za sekondari lakini leo kila kata ina shule ya sekondari na nyingine zaidi yamoja na akina mama wanajifungulia vituo vya afya na hospitali.
 
Kallia alifafanua kuwa Mwalimu Nyerere aliweka misingi ya usimamizi wa elimu wakiwemo viongozi wengine waliofuata baada yake na sasa Rais John Magufuli anatoa elimubure huku wazazi wakibaki kuangalia mahitaji mengine ya watoto, malezi na nidhamu.
 
“RaisMagufuli amenunua ndege lakini wapo wanaopinga hazina maana, si lazima tuzipande wote la hasha.Wataokazipanda watalipa nauli na serikali itaongeza shule nyingine na kutoa huduma zingine kwa wananchi,”alisema Kalli.

Alielea kuwa elimu wanayoitafuta itawapa heshima  wanafunzi haona hivyo hawana budi kujibibidisha kwenye masomo ili wapatikane wana sayansi wakumrithi Rais Magufuli, maprofesa,madaktari na watalaamu wa kada zingine lakini pia wajenge uzalendo kwa nchi yao kabla  na baada ya masomo .

Aidha,Kalli ambaye alikuwa shuleni hapo kushiriki na wanafunzi wa klabu ya Jogging kufanya mazoezi ya kujenga mwili alitumia fursa hiyo kuwaasa wanafunzi hao pamoja na jamii kufanya mazoezi yakuimarisha miili yao na kujenga afya ili kuepukana na maradhi

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post