WABUNGE WATATU CHADEMA WASHIKILIWA POLISI BAADA YA KUJISALIMISHA....KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

Wabunge  watatu wa CHADEMA wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kufuatia amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotaka wabunge wanne wa chama hicho wakamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana.

 
Wabunge waliokamatwa jana Novemba 18, 2019 ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa huku  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee yeye alishakamatwa wiki iliyopita
Heche na Msingwa walikamatwa jana mara baada ya kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuonana na Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza kesi inayowakabili, Thomas Simba.
Wabunge hao wameunganishwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee katika kituo hicho cha Osterbay huku Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya akidaiwa kuwa anaumwa na amelazwa.
Novemba 15, mwaka huu 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru wabunge hao wanne wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo baada ya kutokufika mahakamani hapo bila ya kutolewa taarifa yoyote wakati kesi yao ya uchochezi ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.
Kesi hiyo inatarajia kuendelea leo Novemba 19, 2019 kwaa ajili ya kuendelea na hatua ya usikilizwaji.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post