TCRA YAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE YA SEKONDARI ILBORU


 Mkuu wa kanda ya Kaskazini Imelda Salum akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya vifaa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ilboru iliyopo Mkoani Arusha.
 Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizungumza na wageni waalikwa na wanafunzi katika shuke ya Sekondari Ilboru katika hafla ya Makabidhiano ya vifaa vya Tehama vilivyotolewa na TCRA.
Mkurugenzi mtendaji wa Ausha DC Alvera Ndabagoye akizungumza katika hafla hiyo Wakikadidhiana karatasi za  Makabidhiano ya vifaa kati ya Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Mhandisi Imelda Salum pamoja na Mkuu wa Shule ya Ilboru Dennis Otieno yakiendelea
Uwekaji sa saini katika karatasi za makabidhiano kati ya Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Mhandisi Imelda Salum pamoja na Mkuu wa Shule ya Ilboru Dennis Otieno yakiendelea .
Wakibadilishana karatasi za makabidhiano kati ya Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Mhandisi Imelda Salum pamoja na Mkuu wa Shule ya Ilboru Dennis Otieno yakiendelea ,Wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega na Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha 
 Baadhi ya washiriki katika hafla hiyo katika ukumbibwa shule hiyo
Mkuu wa Shule ya sekondari ya ILBORU Dennis Otieno akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na TCRA.

Na.Vero Ignatus,Arusha 

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini(TCRA) imekabidhi vifaa vya TEHAMA katika shule ya Sekondari ya Ilboru iliyopo mkoani Arusha ambapo kigezo kikubwa ni ufaulu na kushika nafasi ya juu katika ngazi ya Taifa. 

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Mkuu wa kanda ya Kaskazini Mhandisi  Imelda Salum ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi mkuu wa TCRA Nchini Mhandisi James Kilaba amesema kuwa Mamlaka hiyo ina jukumu la kuhakikisha kuwa mawasiliano yanawafikia wananchi wale waliopo mjini na wale waliopo nje ya mji bila kusahau makundi yenye mahitaji maalumu.

''TCRA imeweka imeweka katika mpango mkakati wake utaratibu wa kusaidia utoaji wa vifaa vya vifaa vya Tehama kwa wenye mahitaji makundi maalumu kwa kuzingatia vigezo mbalimbali vinavyopangwa katika kila mwaka wa utekelezaji''alisema Mkuu wa Kanda.

Amesema lengo kuu la kutoa vifaa kwa wanafunzi ili waweze kutumia huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,katika kusaidia kupata mahitaji yao ya kimasomo, kama vile vitabu kwenye mtandao na rejea mbalimbali,sambamba na kutoa chachu katika kufikisha,kurahisisha upatikanaji kwa waalimu na wanafunzi,kuandaa masomo,kuwawezesha kuweka habari za shule kwenye mtandao.

Ametoa wito kwa uongozi wa shule hiyo kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vya TEHAMA vinatumika katika matumizi salama ya mtandao ili yaweze kuleta tija kama ilivyokusudiwa,kwani vikitumika vibaya ni hasara.

''Naomba niweke msisitizo kwenye suala zima la matumizi salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na matumizi sahihi salama ya mtandao,kwani mtandao ukitumika vizuri ni jambo zuri na lenye manufaa sana,lakini ikitumika vibaya ni hasara''Alisema Mhandisi Imelda.

Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega ameishukuru TCRA kwa kutoa vifaa hivyo katika shule hiyo Maalumu ya ILBORU,ambapo ametoa wito kwa walimu na wanafunzi kujitahidi kutumia vifaa hivyo kwa makusudi maalum yaliyokusudiwa huku akiwataka kuvitunza vifaa hivyo ili vidumu.

Kwitega mesema kuwa Mkoa wa Arusha umejipanga kuboresha ufaulu katika shule zake na kuhakikisha kuwa ufaulu unakuwa nzuri kuanzia ngazi ya Kata hadi Kitaifa ili kuleta sifa njema.  

Pia amewaagiza Tehama ngazi ya mkoa kutoa sapoti ya kiufundi kwaajili ya kusaidia vifaa hivyo viendelee kufanya kazi kwa manufaa ya Elimu.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya seondari ya Ilboru Dennis Otieno ameishukuru TCRA kwa kuwapatia vifaa hivyo vya TEHAMA na ameahidi kuwa watavitumia kwa matumizi sahihi yaliyokusudiwa huku akisema vitawasaidia kutuma matokeo ya wanafunzi kwa wazazi,sambamba na wanafunzi kutumia vifaa hivyo kwaajili ya kujisomea na kufahamu mambo mbalimbali bila kuvunja sheria ya mtandao.

''Hapa shuleni tunao wanafunzi ambao ni watundu sana  katika mambo ya mtandao,kunammoja aligundua kifaa cha kutambua kama mwanafunzi anayo simu shuleni na  mwingine aligundua kifaa cha kutambua kama mwanafunzi anaumwa ambapo taarifa zinatumwa mapema kwa mzazi,hivyo kwetu sisi kupata vifaa hivi ni faraja  sana.''Alisema mkuu wa shule

Katika mwaka wa fedha 2018/2019, Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imeshatoa vifaa kwa shule tano nchini kwa kuzingatia vigezo vya ufaulu,matokeo ya mtihani wa Taifa mwaka 2015,ambapo shule ya Ilboru ni miongoni mwa shule hizo zilizofanya vizuri kitaifa na hivyo kuweza kukidhi mahitaji ya kupewa vifaa vya TEHAMA.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Computer,UPS,Printer,utengenezaji wa tovuti za shule pamoja na kuunganisha kwenye mtandao ambapo vifaa hivyo viliwasilishwa na kufungwa shuleni hapo mnamo mwezi Agosti mwaka huu

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post