TCRA WATOA ELIMU KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM- KILIMANJARO


 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akisalimiana na  Katibu wa chama cha Viziwi mkoa wa Kilimanjaro Christina Shirima .Picha zote na Vero Ignatus.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akipeana Mkono na Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiendelea kusalimia na watu wenye mahitaji maalum leo katika Semina ya Siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Kanda ya Kaskazini (TCRA )
Baadhi ya Watumishi wa Malaka ya Mawasiliano Nchini Kanda ya Kaskazini kutoka katikati ni Mhandisi Mwandamizi Jan Kaaya,Wa kwanza kulia ni Lucy Mbogoro Afisa Masoko ,pamoja na Oswarld Octavian wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano Mkoani Kilimanjaro ilipofanyika Semina hiyo ya siku moja ya watu wenye mahitaji malum.
Watu wenye  mahitaji maalumu wasioona na Viziwi wakiwa ukumbini tayari kwa kupatiwa elimu juu ya Umuhimu wa kusajili laini za simu kwa njia ya alama za vidole.
Mafunzo yakiendelea katika ukumbi wa ofisi ya mkoa wa Kilimanjaro leo.
Mkalimani akiendelea kuwatafsiria watu wenye mahitaji maalumu wasiosikia kile kinachoendelea katika mafunzo hayo ya siku moja yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya Kaskazini TCRA.
Watu wenye mahitaji maalumu wasisikia wakiwa makini katika mafunzo kama wanavyoonekana katika picha.

Baadhi ya watu wenye ulemavu wa kutokuona (vipofu)wakiwa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa ma Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kanda ya Kaskazini yaliyofanyika leo Mkoani Kilimanjaro.
Makundi mawili ya watu wenye ulemavu Viziwi na Wasioona Vipofu wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira.

Na.Vero Ignatus,Kilimanjaro.

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA Kanda ya Kaskazini imefanya mkutano wa siku moja na wadau wa mawasiliano wenye mahitaji maalum ,wakiwa katika makundi mawili viziwi na walemavu wa kutokuona .

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Mkoani  Kilimanjaro  Mhandisi Mwandamizi kutoka TCRA kanda ya kaskazini Jan Kaaya  amesema lengo kuu ni kutoa elimu hususani  usajili wa kutumia alama za vidole.

Kaaya amesekuwa  walemavu wasioona na kusikia kutokana na mahitaji waliyonayo kwamba ni kundi ambalo linaweza kusahaulika kirahisi kutokana na hali zao,hivyo Mamlaka hiyo ikaamua kuwapa elimu ili watambue majukumu  na wajibu wa kusajili laini zao simu.

Akifungua Semina hiyo siku moja Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amesema matumizi ya simu yasiwe mzigo kwa wananchi haswa kwenye eneo la mihamala ya fedha.

"Tunajua makampuni ya simu yatahitaji fedha kwaajili ya uendeshaji lakini isiumize wananchi bali iwe gharama nafuu." Alisema mkuu wa mkoa.

Ameyataka makampuni yote ya simu kuangalia uwezekano wa kupeleka mawasiliano vijijini kwani maeneo mengi wananchi wanateseka  kutoka kata kwenda  nyingine kwenda kingine kufuata mawasiliano.

Amesisitiza kuwa ni ukweli usiopingika kwamba asilimia kubwa ya mazao tunayotumia mijini yanatoka kijijini,hivyo vijijini wanahitaji huduma ya mawasikiano kwa asilimia ya juu zaidi kuliko mijini

"Jana nilikuwa kijiji cha Vudee wilaya ya Same watu wanatoka kata moja  hadi nyingine sehemu yenye mnara ili wapate mawasiliano jambo ambalo ni usumbufu  mkubwa kwa wananchi,nyie makampuni ya simu litazaneni jambo hili.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha wasiosikia mkoa wa Kilimanjaro Christina Shirima ameishukuru TCRA kwa kuwapatia elimu hiyo,pia amesema changamoto kubea waliyonayo ni kushindwa kupata vitambulisho vya NIDA kwa hivyo kukwamisha zoezi la kusajili laini zao za simu kwa wakati.

"Nashindwa kuelewa kwanini hivi vitambulisho vya NIDA vinachekewa kwetu sisi au kwa vile sisi ni walemavu !aliuza mlemavu asiyesikia Ahadiel Sowene Mphuru.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post