RC MAKONDA AWAAPISHA WAJUMBE WA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA WILAYA YA KINONDONI NA TEMEKE

NA K-VIS BLOG

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amewaapisha Wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Wilaya ya Kinondoni na Temeke.
 
Kwa upande wa Wilaya ya Kionondoni, walioapishwa ni pamoja na Bw. Derek Murusuri, Balozi Celestine Christopher Liundi na Mama Merina Mlunde.
Aidha Mheshimiwa Makonda pia aliwaapisha wajumbe wengine wane wa Wilaya ya Temeke.
 
 Akitoa nasaha zake baada ya zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa Mhe.  Makonda aliwataka Wajumbe hao kuwa sehemu ya utatuzi wa migogoro na sio kuichochea.
Aliwataka Wajumbe hao kutumia mbinu zote kutatua migogoro ya ardhi ili mashauri yasiwe yanachukua muda mrefu.
 
"Muwe msaada kwa watu wote na hasa wanyonge, wajane na yatima ili wapate haki yap," alisisitiza.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (kulia), akimuapisha Bw. Derek Murusuri kuwa Mjumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Wilaya ya Kinondoni. 
 Mhe. Makonda akimkabidhi kitendea kazi Bw. Murusuri mara baada ya kumuapisha.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul makonda (katikati) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Abubakar Kunenge (wapili kushoto), wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe hao baada ya kuwaapisha.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post