Mwina Kaduguda Apewa Rungu Simba SC


Mwina Kaduguda.
BODI ya Wakuru­genzi ya Klabu ya Simba, im­emteua Mwina Kaduguda kuwa kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo.

Kaduguda anakaimu nafasi hiyo baada ya mwenyekiti aliyechaguliwa na wanachama, Swedy Mkwabi kujiuzulu nafasi yake hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na klabu hiyo kwenye vyombo vya habari jana, ilisema Kaduguda ambaye ni mjumbe wa bodi ya klabu hiyo atakaimu nafasi ya mwenyekiti ikiwa ni uteuzi uliofanywa na bodi chini ya ibara ya 50 ya Katiba ya Simba ya mwaka 2018.

Aidha katika taarifa hiyo, ilisema Bodi ya Wakurugenzi imemteua Salim Abdallah ‘Try Again’ kuwa makamu mwenyekiti wa bodi hiyo.

Katika hatua nyingine, imetajwa kwamba tarehe ya uchaguzi wa kujaza nafasi ya mwenyekiti itatangazwa hapo baadaye na Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo.

Katibu mkuu wa timu hiyo, Arnold Kashembe, alithibitisha uteuzi huo kwa kusema: “Ni kweli uteuzi umefanyika na kumtangaza Kaduguda kuchukua nafasi ya Mkwabi aliyejiuzulu.”
STORI NA WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post