MAAFISA TCRA WAENDELEA KUCHANJA MBUGA KAMPENI YA MNADA KWA MNADA HADI MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI, WAKAZI NJOMBE WAFURIKA KUJISAJILI

Foleni ya Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako na viungo vyake wakiwa katika mistari ya kupata namba za vitambulisho vya Taifa
Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa TCRA Asajile John akizungumza na Wananchi wa Makambako wakati wa usajili wa laini za simu kwa alama.
Add caption
Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akizungumza na Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada wa Uhamasishaji wa Wananchi kujisajili laini za simu kwa alama za vidole.
::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Wakazi wa Makambako mkoani Njombe na viunga vyake  wamejitokeza katika kupata namba za vitambulisho vya Taifa ili kukidhi matakwa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA ipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya  Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.


Kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika maeneo ya miji na Mkoa lengo Wananchi kutumia fursa ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole ambayo unakwenda nchi nzima

 Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini  wa TCRA  Asajile John   amesema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe katika Mji Mdogo wa Makambako kufika katika Viwanja vya idara ya maji kupata namba ya kitambulisho cha Taifa katika mfumo wa NIDA.

 Amesema katika Kampeni hiyo imekuwa inafanywa na kanda hiyo ili kila mwananchi aweze kuwa na namba ya vya Taifa au kuwa na kitambulisho kutokana Ushirikiano na NIDA kuwa katika Kampeni hiyo.

John  amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa kwa pamoja huduma za mawasiliano pamoja na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika  huduma  za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda ulioabakia ni mdogo hivyo kila mtu atumie kutafuta taarifa zinazokidhi usajili wa laini kwa alama za vidole.

Hata hivyo amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Hata hivyo amesema kuwa  kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana  makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

Amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa.

Amesema  TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31 na muda uliobakia ni mdogo tangu tangazo lilipotolewa.

"TCRA tutahakikisha tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema.John

Ameongeza kuwa  Kampeni hiyo imeanza kwa Mikoa yote iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wananchi wameitikia kwa kujitokeza kwa wingi  kuangalia namba  vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.
Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post