LUGOLA: SIKU ZA MTU ANAYEJIITA KIGOGO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII ZINAHESABIKA


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amesema kuwa hivi karibuni Jeshi la Polisi litamtia nguvuni mtu anayejiita kigogo kupitia ukurasa wa Twitter.
Ametoa kauli hiyo leo Novemba 2, 2019 katika mkutano na wanahabari wakati akitoa tathimini ya hali ya usalama hapa nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo amesema kuwa muda si mrefu polisi watamtia nguvuni mtu huyo.
"Kalenda inazo tarehe, utahesabu mwezi mfupi na mrefu, nataka niwaambie kwa kifupi siku za huyo Kigogo zinahesabika na hana siku nyingi", amesema Waziri Lugola.
Aidha katika hatua nyingine, Waziri Lugola ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa na utulivu na amani na kutoa onyo kwa yeyote atakayekuwa na mpango wa kuvuruga uchaguzi ama kampeni basi atatumbukizwa kwenye gari lenye maji ya kuwashawasha.
''Niwaonye wanasiasa, siasa za majitaka na lugha ya matusi zinazoudhi wengine, Jeshi la Polisi limejipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kuwashusha kwenye majukwaa ili wasiendelee kumwaga sumu inayohatarisha amani kwa wananchi", amesema.
"Ole wake yule mwenye mpango wa kuvuruga kampeni au uchaguzi tutamshughulikia, tuna magari ya washawasha, wakorofi na watakaoleta fujo watawashwawashwa kweli, hatutawamwagia tu bali wakorofi kabisa tutawatumbukiza na kuwakogesha kwenye hayo maji yanayowashawasha'', ameongeza Kangi Lugola.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post