![]() |
| Charles Panga |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
MCHAKATO wa
uchaguzi mdogo kujaza nafasi ya mwenyekiti wa chama cha Mapiduzi CCM
mkoa wa Arusha ambayo hadi sasa inashikiliwa na Mkuu wa mkoa wa Morogoro
Lotha Sanare umefungwa leo ambapo zaidi ya wagombea 40 wamejitokeza
kuomba nafasi hiyo.
Uchaguzi huo
unakuja baada ya Nafasi hiyo kuwa wazi kutokana na mwenyekiti
aliyekuwepo Loatha Sanare kuchaguliwa kuwa mkuu wa mkoa wa morogoro
mapema mwezi wa kumi mwaka huu
Mchakato huo
ambao ulianza November 25 umevuta hisia za waombaji wa nfasi hiyo ambao
wameonyesha hamasa kubwa wakati wa kuchukuwa na kurudisha fomu licha ya
uongozi wa mkoa wa chama hicho kutotaja majna hadi sasa.
Licha ya kuwepo
uchaguzi huo mdogo hadi wagombea wanarudisha fomu zao za kuomba nafasi
hiyo chama hicho kimekuwa kwenye usiri mkubwa tokea siku ya mwanzo ya
kutoa fomu hadi leo siku ya mwisho ya kurudisha fomu hizo
Akiongea na
vyombo vya habari mapema leo mara baada ya kurudisha fomu mmoja ya
wagombea wa nafasi hiyo Charles Panga ambaye ndiye mgombea kijana zaidi
kati ya waliogombea nafasi hiyo alisema kuwa umri sio tatizo la uongozi
bali mawazo ya kiuongozi na utendaji ndio silaha kubwa kwa mwanasiasa.
Alisema kuwa
amejipanga pindi atakapopitishwa kwenye uchaguzi huo kuhakikisha chama
hicho kinaisimamia serikali kutekeleza ilani ya chama hicho 2020 na kuwa
daraja la wananchama wapya kuweza kuongoza kwa vitendo na kuacha siasa
za kizamani za makundi ndani ya chama hicho
“Nitakuwa sehemu
ya kukipigania chama changu na wakati wote nitakuwa tayari kupokea
maelekezo ya kufikia sehemu ya kuendelea chama change kushika dola na
kushinda chaguzi mbalimbali”alisema Panga.
Alisema kuwa
chama hicho pindi akipata ridha hiyo atasaidiana na viongozi kuhakikisha
kuwa wananchi na wanyonge kero zao zinashughulikiwa kwa kuwa chama ndio
mtetezi wa wananchi hao naye kuwa sehemu ya kuwasaidia wananchi kufikia
malengo hayo.
Uchaguzi huo
unatarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo au mwishoni mwa wiki ambapo hadi
sasa wananchama wa chama hicho wapo mkao wa kula kuhakikisha wanampata
mwenyekiti wao wa mkoa katika uchaguzi huo.
Duru za kisiasa
mkoani hapa zimejikita kwa wagombea kuhakikisha wanapata mwenyekiti
sahihi wa kuvaa viatu vya Loatha Sanare ambaye utendaji wake ulimfanya
mwenyekiti wa chama hicho Taifa na Rais Dkt.John Magufuli kumchagua kuwa
mkuu wa mkoa wa Morogoro kuchukuwa nafasi ya Dkt. Kabwe Stephen na
hivyo kuvutia wagombea zaidi ya 40 hadi dirisha lilipoungwa saa kumi
jioni November 27
