KIJANA ALIYEMTISHIA MWENZAKE KWA BASTOLA YAMKUTA MAZITO....IGP AMTAKA AJISALIMISHE POLISI


Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amemtaka kijana aliyemtishia mwenzake bastola kuripoti polisi baada ya kuonekana akifanya kitendo hicho katika picha za video zinazosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini.

Mbali na kuripoti, Sirro amesema anatakiwa kusalimisha silaha yake.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Utatu inayolenga kukomesha rushwa barabarani.

Sirro amesema ameagiza kukamatwa kwa kijana huyo lakini amekuwa akipiga chenga,  amemtaka akajisalimishe mwenyewe kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post