DKT.NDUMBARO AIPONGEZA NISHATI KUWA YA KWANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti  ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurian Ndumbaro( aliyesimama) akizungumza na washiriki wakati akifunga Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kilichofanyika mkoani Tanga
.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati, Raphael Nombo(kushoto) akizungumza na Washiriki wa Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake(hawapo pichani) kabla ya kufungwa kwa kikao hicho.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti  ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurian Ndumbaro( katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake , baada ya kufunga kikao hicho kilichofanyika mkoani Tanga.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti  ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurian Ndumbaro( kushoto) akiwa amembatana na Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake ambao wanaofanya kikao kazi mkoani Tanga ,kilichofungwa na Katibu Mkuu huyo.
Meneja Mkuu wa Kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania,( GASCO), Mhandisi Baltazar Mroso akitoa neno la Shukrani baada ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti  ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurian Ndumbaro, kufunga kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake

Na Zuena Msuya, Tanga

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti  ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurian Ndumbaro ameipongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake kwa kuwa ya kwanza  kutekeleza agizo la Rais kwa kufanya vikao vya pamoja vya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utumishi wa umma ,utendaji kazi na utawala bora kati ya watumishi, wafanyakazi pamoja na viongozi katika sehemu za kazi.

Dkt. Ndumbaro alisema hayo Novemba 15, 2019, wakati akifunga Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kilichofanyika mkoani Tanga.

Alisema kuwa kwa kufanya mikutano ya namna hiyo, ni dhahiri Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake imelenga kutekeleza agizo la Rais na dhima ya serikali inayoelekeza  utumishi wa umma wenye uwajibikaji, uadilifu, unaofanya kazi kwa juhudi na maarifa,uzalendo, na ule ambao watumishi wake wanakuwa na sifa stahiki.

Dkt. Ndumbaro alisema kuwa Wizara ya Nishati inatekeleza agizo hilo kwa kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Wizara na Taasisi zilizochini yake kwa lengo la kuboresha utendaji kazi, utumishi wa Umma na Utawala bora sehemu za kazi.

Alisema kuwa utumishi wa umma unaozingatia misingi yake hujenga utawala bora kwa taifa na wananchi wake, kwa kuimarisha mahusiano mazuri kati ya wananchi, watumishi wa umma, wafanyakazi pamoja na viongozi katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kupata matokeo chanya kwa taifa na wananchi wake.

Sambamba na hilo alisema kuwa wizara hiyo na taasisi zake inatekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi na taifa, hivyo kuwepo kwa utumishi wa umma wenye kuzingatia misingi imara sehemu za kazi ni chachu ya kuongeza ari ya watumishi katika kila sekta kufanya kazi kwa bidii na kujituma bila kuchoka na kuweka mbele uzalendo na maslahi taifa.

Aliwaelekeza wasimamizi wa rasilimaliwatu kutoa motisha kwa watumishi au wafanyakazi  wanaofanya kazi vizuri kwa kuwapatia vyeti au barua maalumu ya utambuzi ambazo zitaweka katika eneo la mapokezi ili kuinua ari ya kufanya kazi kwa bidii kwa kila mtumishi au mfanyakazi, na pia kutoa adhabu ya namna hiyo kwa wale ambao hawafanyi vizuri kazini.

Aliwasisitiza watumishi wa umma kutofanya kazi kwa mazoea na kwamba watambue kuwa mtumishi wa umma unaweza kufanya kazi katika ofisi yoyote ya umma iliyopo nchini, na kwamba wasikariri kuwa watakaa sehemu moja siku zote.

“Watumishi wa umma muwe na tabia kama ya kuvaa na kuvua makoti tofauti, kwa maana leo utakuwa katika kutuo cha kazi A, kesho utapelekwa Y, au P na baadaye G, huu ni utaratibu uliowekwa kwa manufaa ya kujenga na kuboresha utumishi wa umma”,alisisitiza  Dkt.Ndumbaro 

Aidha aliendelea kukumbusha kuwa watumishi pamoja na wafanyakazi wapewe nafasi za kwenda kusoma yale yenye tija kwa wizara ama taasisi husika, na mafunzo hayo yatolewe kwa watu wote wa kila idara na siyo kupendelea mtu mmoja.

Vilevile alirudia kuwaeleza watumishi wa umma kuendelea kutunza siri za serikali na kulinda mali ya umma bila kusahau kupiga vita vitendo vya rushwa.

Katika zoezi linaloendelea la kuhakiki watumishi wa umma, serikali imebaini kuwa kuna watumishi ambao majina yaliyopo katika vyeti walivyosomea na majina katika barua walizoajiriwa ni tofauti, hivyo wanaendelea kufanya utafiti kwa kushirikisha vyombo vya serikali ili kubaini kama vyeti hivyo ni vya watumishi hao kihalali au ni vya watu wengine ili waweze kutoa maamuzi sahihi wakati ukifika.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post