DIAMOND PLATNUMZ AMJIBU ALI KIBA


Diamond Platnumz amezungumzia kilichoandikwa na msanii mwenzake, Ali Kiba katika mtandao wake wa  kijamii wa Instagram saa chache baada ya  kumualika kushiriki tamasha la Wasafi litakalofanyika Novemba 9, 2019.
Akizungumza jana Ijumaa Novemba Mosi, 2019 katika televisheni ya Wasafi ,Diamond alisema hakujua Ali Kiba alilenga nini, akibainisha kuwa hawezi kuwa na chuki naye.“Alikiba ni kaka yangu, amenizidi umri na alianza muziki kabla yangu. Sijui aliandika vile akimaanisha nini, yeye na mimi ni miongoni mwa tunaoiletea sifa nchi kupitia muziki, upinzani wetu ni kwenye muziki tu, simchukii na nina imani naye pia hanichukii.

“Mimi nimetokea maisha ya chini sana ila Mwenyezi Mungu amenibariki ndio maana niliwashika mkono watu wengine ikiwemo Harmonize, tamanio la WASAFI ni kuona vijana tunapeana support na kumuunga mkono kwenye vitu ambavyo anavifanya.
“Mtu anavyofanikiwa na kuanza kushika mkono vijana wengine ni jambo zuri, furaha yangu ni kuona vijana wengi wa Tanzania wenye talent wanafanikiwa, pengine na mimi nisingemshika mkono, watu wasingeona kipaji chake.
”Nimefanya kazi nyingi za Kushirikiana na wasanii, nina collabo nyingi ndani hadi natamani nizitaje, nina ngoma inakuja na Swaelee, kuna nyingine nimefanya na Steff London.
“Wasafi Festival itaanza mapema na kutakuwa na mashindano ya kuimba, Mshindi atapata Tsh. Millioni 10 na nafasi ya kusainiwa WCB Wasafi, kutakuwa na mashindano ya Dancers ambapo washindi pia watapata zawadi ya Tsh. Million 10 na nafasi ya kufanya kazi na wasanii wa WCB.
“Juzi tu hapa nilishinda Tuzo ya Mtumbuizaji bora Siku ya Festival nitatumbuiza kweli na hapa Nipo na Mh. Makonda Siwezi kumuangusha kwenye mkoa wake,” amesema Diamond.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post