CCM NAO KUTOA TAMKO KESHO KUTWA KUHUSU UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema chama hicho kwa sasa kinaendelea kufuatilia muenendo wa zoezi zima la uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na kinatarajia kutoa tamko lake Novemba 13, 2019.

Polepole ametoa kauli hiyo Leo Novemba 11, 2019 kupitia ukurasa wake wa Twitter, huku zoezi zima la uchaguzi huo likiwa limekumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo wagombea wengi wa vyama mbalimbali kuenguliwa.

Kutokana na changamoto hizo, jana Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo alitengua maamuzi yote na kuamua kuwaruhusu wagombea wote nchini waliochukua fomu na kuzirejesha kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa bila kujali kama walienguliwa isipokuwa kwa wale wasio raia wa Tanzania, hawakujiandikisha au wamejiandikisha mara mbili.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post