BREAKING NEWS: PROFESA ASSAD OUT!! RAIS MAGUFULI ATEUA CAG MWINGINE


Na Mwandishi Wetu, APC BLOG DSM
 Rais Magufuli leo Novemba 3, 2019 amemteua Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Uteuzi huo unaanza kesho, Kichere anachukua nafasi ya Profesa Mussa Assad ambaye kipindi chake cha uongozi cha miaka mitano kinaishia kesho.
Mteule huyo ambaye alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), alitenguliwa uteuzi wake na Rais Magufuli ambaye alimteua tena kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Juni 8, mwaka huu.
Akisoma taarifa ya uteuzi huo leo Jumapili Novemba 3, 2019, Balozi John Kijazi amesema nafasi ya Kichere itajazwa na Katarina Revocati ambaye alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.
Pia, Rais Magufuli amewateua Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Kanali Francis Mbindi kuwa kamishna wa kazi ofisi ya Waziri Mkuu na majaji 12 wa Mahakama Kuu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post