MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amewataka wenyeviti
wa Vijiji, vitongoji na mitaa waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za
mitaa uliopita wasiwe chanzo cha migogoro kwa wananchi kwa kugeuka wauza ardhi
bali wahakikishe wanashirikiana nao kutatua kero zinazowakabili.
Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji aliyasema wakati mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani
ambapo alisema lazima watambue dhamana kubwa walioibeba ni kuhakikisha wanakuwa
mstari wa mbele kuchochea maendeleo kwenye maeneo yao.
Alisema kwamba wananchi wanataka maendeleo ndio maana
wamewachagua hivyo wanajukumu kubwa la kutekeleza hayo kwa vitendo ikiwemo
kutetea maslahi yao pindi wanapokumbana na changamoto mbalimbali.
“Unapokuwa kiongozi lazima utetee maslahi ya wananchi
wako pia utembue changamoto zinazowakabili hapa kipoumbwi asilimia kubwa wananchi
shughuli zao na uvuvi hivyo Mwenyeviti mpya wa hapa kuwa imara kusimamia wavuvi
waweze kuvua kwa usalama wapate ridhiki yao ya halali”Alisema Aweso.
Mbunge huyo pia aliwaambie wananchi kwamba hakuna
demokrasia yoyote ya kutafuta viongozi kwenye Taifa hili zaidi ya uchaguzi
hivyo vikiwemo kuwataka iongozi ambao wamepatikana watambue kwamba wana
kipumbwi na wana Pangani wanahitaji maendeleo na sio jambo jingine.
Hata hivyo pia aliwataka pia hakikisha kila baada ya
miezi mitatu wanasoma mapato na matumizi huku akiwaambia kwamba sio wakati
ukiwa umefika hata simu zao hazipatikani kwa kuwaeleza huo utakuwa sio
uoingozi.
“Wapo watu wamewaaminisha watu kwamba CCM ikiingia hapa
Kipumbwi watateseka hawataleta maendeleo…lakini wapo watu wanasema baada ya CCM
kuingia hapa eti boti zitafukuzwa hafukuzwi mtu hapa “Alisema Mbunge huyo.
Mbunge huyo aliwataka viongozi hao kufanya kazi kwa
bidii ili kuweza kuwapa maendeleo wananchi hao maana hawana wenyeviuti wengine
zaidi ya nyie.