ASASI YA KIRAIA YATOA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA KATIKA MAGEREZA YA ARUSHA, TANGA NA KILIMANJARO

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP –  Phaustine Kasike akisalimiana na Meneja Miradi wa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bw. Charles Shang’a alipowasili katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa na Asasi hiyo kwa ajili ya  wafungwa  leo Novemba 15, 2019

.
Meza kuu wakiongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike (wa pili toka kushoto) wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania ikiashiria ufunguzi wa hafla fupi ya kupokea misaada ya Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa iliyotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ. Tukio hilo limefanyika leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi.
Kaimu Mkurugenzi wa Asasi ya Dorcas Aid International Tanzania Bw. Joseph Kumwembe akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi msaada wa Kibinadamu kwa ajili ya Wafungwa nchini. Dorcas Aid International Tanzania hushirikiana na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ katika kutoa misaada ya namna hiyo.
Kamishna Jenerali wa Magerezanchini, CGP – Phaustine Kasike akitoa hotuba kwa wageni mbalimbali (hawapo pichani) waliohudhuria hafla fupi ya kupokea msaada wa Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa  kutoka kwa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ  leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi.
 Kamishna Jenerali wa Magereza  nchini, CGP – Phaustine Kasike akipokea msaada wa baiskeri ya walevu pamoja na vitu mbalimbali  vilivyotolewa  na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ leo Novemba 15, 2019 kwa ajili ya wafungwa. Hafla ya upokeaji wa misaada hiyo imefanyika katika gereza Kuu Karanga Moshi.
Muonekano wa baadhi ya misaada ya Kibinadamu iliyotolewa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ iliyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi. Misaada imekabidhiwa leo kwa ujumla wake ina thamani ya zaidi ya milioni 183.
Mhandisi ujenzi wa Jeshi la Magereza, SP. Julius Sukambi akitoa maelezo ya kitaalam kwa Kamishna Jenerali wa Magerezanchini, CGP – Phaustine Kasike alipotembelea katika eneo hilo la ujenzi wa Kiwanda Kipya cha bidhaa za ngozi kinachojengwa nje ya eneo la Gereza Kuu Karanga, Moshi
(Picha zote na Jeshi la Magereza).
…………………..
Na ASP Lucas Mboje, Moshi

ASASI ya Kidini ya New Life In Christ imekabidhi kwa Jeshi la Magereza misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 183 ambayo itawanufaisha wafungwa na Mahabusu waliopo magerezani katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga. 

Akizungumza kabla ya kukabidhi misaada hiyo ya wahalifu waliopo magerezani, Kaimu Mkurugenzi wa Asasi ya Dorcas Aid International Tanzania, Bw. Joseph Kumwembe amesema vifaa vilivyokabidhiwa ni magodoro, sabuni, nguo za watoto, mabranketi, vipeperushi, vifaa vya usafi na vitabu vya kiroho.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ameishukru Asasi hiyo isiyo ya Kiserikali kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza kwa ukamilifu utoaji wa misaada ya kibinadamu pamoja na baadhi ya huduma muhimu kwa wafungwa ikiwemo mafunzo ya Kijasiriamali kwa wafungwa hivyo kulisaidia Jeshi la Magereza katika suala zima la urekebishaji wa wafungwa.

“Niwashukru sana Asasi hii kwa moyo wao wa upendo na kujitolea na niwapongeze sana kwa kutambua kwamba wahalifu waliopo magerezani ni Binadamu kama walivyo Binadamu wengine na wanahitaji misaada ya ki-binadamu kama hii,” Amesema Jenerali Kasike.

Aidha, Jenerali Kasike ametoa wito kwa Asasi nyingine zisizo za Kiserikali kuiga mfano uliooneshwa na New Life in Christ na Dorcas Aid International Tanzania ili ziweze kushirikiana na Jeshi la Magereza kwa manufaa ya Taifa.

Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike amewataka Wakuu wote wa Magereza yaliyonufaika na misaada hiyo kuhakisha kuwa misaada inawanufaisha walengwa kwa maeneo yaliyokusudiwa samabamba na kusimamia vyema vifaa hivyo.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike mara baada ya kupokea misaada hiyo ametembelea eneo la mradi mkubwa wa uwekezaji wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi ambacho ni cha ubia kati ya Jeshi la Magereza pamoja na Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSSSF. Kiwanda hicho kinajengwa katika eneo lililopo nje ya Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo amewasisitiza wakandarasi wa ujenzi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post