AJALI YA LORI YAUA WATU WATATU JIJINI DAR

nde       Saturday, November 23, 2019

Jumla ya watu watatu wamefariki Dunia papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya, baada ya kugongwa na Lori la mafuta lililoacha njia na kuparamia watembea kwa miguu, maeneo ya Mlimani City, lililokuwa likitokea Ubungo kwenda Mwenge.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu, amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 5:20 asubuhi, ambapo mara baada ya ajali hiyo kutokea, dereva alikimbia na kutoweka kusikojulikana.


"Dereva aliacha njia na kugonga watembea kwa miguu, kati ya watu wanne waliogongwa watatu walifariki papo hapo na mmoja ni majeruhi amepelekwa hospitali, mmoja aliyefariki ametambulika kwa jina la Daniel Mushi ni fundi umeme na mkazi wa Kimara - Temboni, ni uzembe tu wa dereva maana aliacha njia na kuparamia watembea kwa miguu" amesema Kamanda Taibu.
Kwa mujibu wa Kamanda Taibu, miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali hiyo na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kufanya juhudi za kumsaka dereva huyo popote alipo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post