ZOEZI LA UANDIKISHAJI ORODHA YA WAPIGA KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAONGEZEWA SIKU TATU HADI OKTOBA 17, 2019

  
  
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

 


 TANGAZO LA MAREKEBISHO YA RATIBA YA UANDIKISHAJI WA ORODHA  
YA WAPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WA MWAKA 2019  
 
(Limetolewa chini ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka mwaka
2019  (Matangazo ya Serikali Na 371, 372, 373 na 374 ya mwaka 2019).

Kwa mujibu wa Kanuni ya 49 ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo (Tangazo la Serikali Na. 371 la mwaka 2019), Kanuni ya 51 ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya 
Mtaa katika Mamlaka za Miji (Tangazo la Serikali Na. 372 la mwaka 2019), Kanuni ya 52 ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za mwaka 2019 (Tangazo la Serikali Na. 373 la mwaka 2019) na Kanuni ya 52 ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji za mwaka 2019 (Tangazo la Serikali Na. 374 la mwaka 2019) Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ana mamlaka ya kutoa miongozo mbalimbali kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 
Tangu tarehe 8 Oktoba, 2019 kumekuwa na zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika Orodha ya Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba, 2019.

 
Zoezi la uandikishaji lilipangwa kumalizika tarehe 14 Oktoba, 2019.  Zoezi hili limeendelea kupata mafanikio makubwa kwani hadi mnamo tarehe 12 October zaidi ya wananchi milioni kumi na moja waliweza kujiandikisha katika daftari la Orodha ya Mpiga Kura za Serikali za Mitaa.
Hata hivyo, kumejitokeza changamoto kuu mbili wakati zoezi la uandikishaji likiendelea. Changamoto hizo ni kama ifuatavyo;
1.    Kumekuwa na mvua nyingi kwa Mikoa  mingi hivyo kusababisha watu wengi kushindwa kujiandikisha kwa wakati. Maeneo mengine baadhi ya kaya zimejikuta zimezingilwa na maji hususani kwa Mkoa wa Morogoro na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya ukanda wa Pwani. 
2.    Baadhi ya wananchi ambao zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura limewapitia hivi karibuni au limekuwa likiendelea katika maeneo yao wamekuwa kichanganya kwamba kwakuwa wamesha jiandikisha katika daftari la kudumu na kupewa kitambulisho cha Mpiga kura wamekuwa na dhana isiyo sahihi kwamba vitambulisho hivyo vitawawezesha kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hata kama hawata jiorodhesha katika daftari la orodha ya mpiga kura kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Dhana hiyo imesababisha baadhi ya wananchi kuchelewa kujiandikisha katika zoezi linalo endelea sasa la uandikishaji kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
 Kutokana na changamoto hizi kuu mbili, na kutokana na misingi ya utoaji  wa haki na kwa kuzingatia masharti ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kama zilivyo ainishwa hapo juu natoa Mwongozo kuwa zoezi la uandikishaji linaongezewa siku tatu zaidi za uandikishaji hadi tarehe 17 Oktoba, 2019 badala ya tarehe 14 Oktoba, 2019 iliyotangazwa awali. 
Kufuatia mabadiliko hayo, ratiba ya uandikishaji wa Orodha ya Wapiga Kura na matukio yanayohusu uandikishaji yatakuwa kama ifuatavyo:
Na.  
TUKIO  
TAREHE  
MHUSIKA  
1.  
Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura    
8-17 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
2.  
Kubandikwa kwa Orodha ya Wapiga Kura  
18 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
3.  
Ukaguzi wa Orodha ya Wapiga Kura    
18-24 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
4.  
Pingamizi kuhusu uandikishaji wa wapiga kura    
18-24 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
Msaidizi  
5.  
Uamuzi kuhusu pingamizi    
24-25 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
Msaidizi  
6.  
Marekebisho ya Orodha ya Wapiga Kura    
24-25 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
Msaidizi  
7.  
Kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa pingamizi
 24-26 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
  
Uamuzi wa rufaa  
24-29 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
  
Matukio mengine ya Uchaguzi hayataathiriwa na mabadiliko haya. 
Kwa Tangazo hili, Wananchi wote wanaombwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Orodha ya Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuwa na sifa ya  kupiga kura katika Uchaguzi huo.  

SELEMANI S. JAFO (MB)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS,
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

13 Oktoba, 2019

 
   

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post