WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI URUSI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumapili, Oktoba 20, 2019) kwenda Urusi kuhudhuria mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi (Russia-Africa Summit), utakaofanyika jijini Sochi, Urusi, Oktoba 23 – 24, 2019.
Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.
Mkutano huo utakaoendeshwa chini ya uenyekiti wa pamoja (Co-chaired) wa Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), unalenga kurejesha na kuimarisha uhusiano baina ya mataifa ya Afrika na Urusi ambao uliyumba baada ya kusambaratika kwa “Union of Soviet Socialist Republic” (USSR) mwaka 1991.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali utafanyika katika sehemu mbili, ambazo ni Kongamano la Biashara (Russia Business Forum) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 23, na Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Urusi na Afrika uliopangwa kufanyika Oktoba 24, 2019.
Waziri Mkuu atashiriki kwenye mikutano yote miwili.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post