Wafugaji kutumia Simu kufuata Malisho na Maji

Mwandishi wetu,Monduli

Wafugaji  wa wilayani tatu za mkoa wa Arusha,watakuwa wakifikia malisho na maji ya mifugo yao kwa kutuma ujumbe wa simu kuulizia eneo lenye maji na malisho na kujulishwa.
Rais wa Shirika la PCI Carrie Hetessler Radelet akizungumza  katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kusasaidi wafugaji kuyafikia malisho na maji kwa kupitia huduma ya Afriscout wilayani Monduli


Kaimu Mkurugenzi wa PCI Jennifer Waugaman akiwa na mratibu wa PCI nchini John Laffa  wakipewa zawadi  baada ya kuzindua mradi huo

Mradi huu umezinduliwa jana na shirika la  kimataifa la PCI ,l, katika kijiji cha Arkaria wilayani Monduli na  utatekelezwa pia wilaya za Longido na Ngorongoro ambazo zina idadi kubwa ya mifugo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais wa PCI, Carrie Hetessler-Radelet alisema, wafugaji kupitia simu zao za mkononi, baada yakupakuwa  application ya Afriscout watatuma   bure ujumbe kwenda15054 kuuliza malisho na maji.

Hetessler –Radalet amesema baada ya kuuliza,mtandao huo utaonesha ramani za sehemu ya maji na malisho ambayo imepigwa angani.

Amesema mradi huo, utawezesha wafugaji kuacha kusafiri muda mrefu kusaka malisho, kuharibu mazingira lakini pia utapunguza vifo vya mifugo na adha ya wafugaji kushindwa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, Jennifer Waungaman amesema mradi huo ambao unatarajiwa kuwanufaisha sana wafugaji.

“tunawaomba wafugaji kutumia huduma hii ambayo pia itawasaidia kusimamia vizuri nyanda za malisho yao”alisena

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu mkurugenzi endeshji wa malisho na vyakula vya mifugo,Dk Asimwe Rwiguza  alisema mradi ho una manufaa makubwa kwa wafugaji na amelitaka shirika hilo kupanua huduma hiyo nchi nzima.

Mfugaji John Laizer amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwao na itaondoa tatizo la mifugo kufariki wakati wa kiangazi na migogoro na wakulima.

Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Monduli,Joseph Rutabingwa alisema halmashauri ya Monduli itaupa ushirikiano mradi huo ili wafugaji wanufaike zaidi.

Mradi huu pia unatekelezwa katika nchi tatu barani ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia na shirika hilo linafanya kazi katika nchi 16 Duniani.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post