Wafanyakazi 10 wa OBC watozwa faini ya Milioni 100 kwa kosa la Kufanyakazi Nchini bila kuwa na Vibali

Na Mwandishi Wetu, Arusha
HAKIMU Mkazi wa Mahakama  ya Wilaya Arusha Rose Ngoka jana amewahukumu washitakiwa kumi ambao ni raia wa kigeni, kulipa Sh.milioni 100  au kwenda jela miezi 12, kwa kosa kufanya kazi kampuni ya uwindaji ya Oterlo Businness Coperation (OBC) bila kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini.

Raia hao  wa kigeni ni  Darweshi Jumma, Riaz Aziz Khan, Mohammad Tayyab, Ali Bakhash, Abdulrahman Mohammed, Martin Crasta, Imtiaz Feyaz, Arshad Muhammad, Hamza Sharif na Zulfiqar Ali.

Image result for waarabu wa OBC
Related image
Mkurugenzi wa OBC Issack Mollel akifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kutokana na mashtaka ya uhujumu uchumi yanayomkabili pamoja na kuajiri raia wa kigeni bila ya kuwa na vibali

Hakimu Ngoka alisema mahakama imewatia hatiani washitakiwa hao kwa kukiri kufanya kosa hilo nchini na kuamuru kila mmoja kulipa faini ya Sh.milioni 10 au kwenda jela miezi 12.

"Lakini kwa kuzingatia maombi ya Wakili wenu wa utetezi Steven Mosha na kwa kuangalia  mazingira ya kesi na madhara ya kijamii kama alivyosema mahakama imekata hatiani na kuwapa adabu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine,"alisema

Ngoka mbali na kuwapa adhabu ya kulipa faini,pia aliwaonya washitakiwa hao na kuwataka kutii sheria,kanuni na taratibu za nchi pindi wanapoingia nchini.

Wakili wa utetezi Steven Mosha kabla ya hukumu hiyo kutolewa aliomba Mahakama hiyo kuwapa adhabu ndogo washitakiwa hao kwa sababu ni kosa lao la kwanza kufanya.

"Lakini naomba iwapunguzie adhabu sababu wamekiri na kuokoa muda wa mahakama,lakini pia washitakiwa wawili wana utaifa wa nchi ya India na nane raia wa Pakstani na walishitakiwa miezi mingi nyuma na kutumia gharama kubwa za kuishi,"alisema

Alisema kutokana na kushitakiwa wamelazimika kutumia fedha nyingi katika kuishi nchini na wengi wao vijana wanahitajika katika taifa lao kujenga taifa.

"Lakini Hakimu naomba wape adhabu ndogo sababu wengine umri wao mkubwa wanahitaji  kukaa wanafamiliya zao,"alisema

Aidha alisema kuwapa adhabu kubwa itasababisha ugumu wa maisha kwa familiya zao,hivyo aliomba wapewa adhabu ya kulipa fedha kwa sababu wapo tayari kulipa kiasi chochote cha fedha ambacho mahakama hiyo itaamuru.

Kabla ya Wakili wa utetezi kutoa  maombi hayo Wakili Mkuu wa Serikali Maritenus Marandu alisema  kabla ya jana washitakiwa hao waliandika barua iliyowasilishwa na Wakili wao Steven Mosha  ikionyesha washitakiwa hao kukiri makosa yao.

Pia aliiambia  mahakamani hiyo kuwa, upande wa Jamuhuri hauna kumbukumbu za makosa ya nyuma,ila aliomba mahakama iwape adhabu inayostahili kulingana na kosa walilofanya.

Akiwakumbusha washitakiwa hao makosa yao Wakili Mwandamizi wa serikali Mkoa wa Arusha Abdallah Chavula akiwa na Wakili Idara ya Kazi Arusha Emmanuel Mweta alisema washitakiwa hao walifanya kosa la kufanya kazi nchini bila vibali vya kazi kati ya  Novemba 2018  na  Januari 2019.

Alisema washitakiwa hao wenye taaluma mbalimbali walikamatwa wakiwa na hatia zao zà kusafiria  wakijiandaa kuondoka nchini.

Washitakiwa hao walikamatwa  Januari mwaka huu na Septemba 2 mwaka huu kesi hiyo  ilifutwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Mfawidhi  Arusha Niku Mwakatobe kutokana na Wakili wa  serikali kutokuwa tayari kuwasomea hoja za awali ili kesi iendelee.

Wakati huo huo mshitakiwa wa kwanza  Isaya  Mollel katika kesi hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa OBC anayekabiliwa  na kosa la kuajiri raia hao wa  kigeni, bila ya kuwa na vibali kwa mujibu wa sheria za nchi za kutoa ajira kwa wageni hajakiri kosa na amepangiwa kesi yake Oktoba 16  mwaka huu.

Washitakiwa hao walifanikiwa kulipa faini hiyo na kuachwa huru.

 Image result for waarabu wa OBC

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post