UMEME UPO WA KUTOSHA WEKEZENI PWANI KATIKA VIWANDA

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wafanyabiasha, wenye viwanda pamoja na wadau mbalimbali ( hawapo pichani) wakati wa maonesho ya wafanyabiashara na wenye viwanda yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.


Naibu Waziri wa Viwanda , Mhandisi Stella Manyanya(kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa habari alipotembelea banda la Shirika la Umeme nchini, TANESCO, wakati wa maonesho ya wafanyabiashara na wenye viwanda yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akisaini kitabu cha wageni alipotebelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini( TPDC) viwanda pamoja na wadau mbalimbali ( hawapo pichani) wakati wa maonesho ya wafanyabiashara na wenye viwanda yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na mmoja wa   wenye viwanda walioshiriki katika maonesho ya wafanyabiashara na wenye viwanda yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(kushoto) na mhandisi Stella Manyanya wakipata maelezo kutoka kwa mfanyabiashara mwenye kiwanda aliyeshiri katika maonesho ya viwanda na wafanyabiashara yaliyofanyika mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo ( kulia), wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanakijiji( hayupo pichani) baada ya kushindwa kufika katika Kijiji cha Kitima wilayani Bagamoyo kilichokubwa na mafuriko,baada ya barabara kuharibika na kujaa maji kufuatia mvua zinazonyesha katika Mikoa ya Ukanda wa Pwani.
…………………..
Na Zuena Msuya, Pwani
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wafanyabiashara, wenye viwanda na wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kujenga na kuwekeza katika viwanda mkoani Pwani kwa kuwa umeme upo mwingi na wa kutosheleza mahitaji ya viwanda hivyo.
Mgalu alisema hayo Oktoba 17,2019 wakati wa ufunguzi wa maonesho ya pili ya wafanyabiashara na wenye viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Pwani, ambapo Mgeni Rasmi katika maonesho hayo alikuwa ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, kwa niaba ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.
Maonesho hayo yanayofanyika kwa siku 7, yamewashirikisha wafanyabisha, wenye viwanda pamoja na  wadau mbalimbali ndani na nje nchini, ambapo zaidi wa washiriki zaidi ya 300 wamejitokeza katika maonesho hayo.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Mhandisi Manyanya aliwahakikishia wafanyabiashara na wenye viwanda kuwa, Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza, pia serikali imeweka mazingira rafiki katika uwekezaji na uwezeshaji wa namna yeyote hususani katika viwanda.
Mhandisi Manyanya pia alisema kuwa, wafanyabiashara na wenye viwanda wasiwe na wasiwasi juu ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa kuwa Tanzania ina miradi mikubwa ya kuzalisha umeme: Akijata visima vya gesi mkoani Mtwara na Lindi pamoja na Mradi Mkubwa wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere kwa kutumia maporomoko ya maji katika Bonde la Mto Rufiji utakaozalisha zaidi ya Megawati zaidi ya 2000 za umeme mwingi ,wa kutosha na wa bei nafuu. 
Akizungumzia hali ya upatikanaji wa umeme kwa Mkoa wa Pwani, Mgalu alisema kuwa kwa sasa mradi mkubwa wa kusambaza umeme katika vijiji 150 unatekelezwa ili kurahisisha usambazaji wa umeme katika viwanda vitakavyojengwa na vinavyojengwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Vilevile Mkoa wa Pwani utanajenga kituo cha kupoza umeme cha Uruguni pamoja  kutanua kituo cha kupoza na kupokea umeme cha Mlandizi na Chalinze ambavyo vitakuwa na njia zake za kusafirisha umeme kwenda viwandani.
Sambasamba na hilo, kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ubungo pia kitatanulia na kuongezewa nguvu na kuzalisha Megawati 800 za umeme kwa lengo la kuimarisha na kuboresha upatikani wa umeme katika wa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani.
Alilitaka Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kuendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji na usambazji wa umeme ili kuepuka changamoto ya kukatika umeme pasipo sababu ya msingi.
Kuhusu malalamiko ya bei ya gesi yaliyokuwa yametolewa na wenye viwanda, Mgalu alitumia hadhara hiyo kuwaeleza wenye viwanda na wafanyabiashara kuwa , Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini ( TPDC) limepewa kazi kusikiliza na kujadiliana na wafanyabiasha na wenye viwanda ili kupata mapendekezo ya kuboresha na kupunguza bei ya gesi kwa manufaa ya watumiaji na  taifa kwa ujumla.
Serikali ilitenga shilingi Bilioni 17 na Dola za Kimarekani milioni 4, kwa ajili ya usambazaji wa umeme katika Mkoa wa Pwani na shilingi bilioni 64 kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme wa Peri Urban katika maeneo 186 mkoani humo, ambapo mahitaji ya umeme kwa sasa ni megawati 82.
Katika hatua nyingine, baada ya kushiriki katika ufunguzi wa manesho hayo, Naibu Waziri Mgalu, aliungana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Kamati ya ulinza na usalama ya mkoa huo, kutembelea maeneo ya kijiji cha kitima wilayani bagamoyo ambayo yamekubwa na mafuriko kufuatia mvua zinazoendela kunyesha katika Mikoa ya Pwani ya bahari ya hindi ikiwemo Mikoa ya Dar es salaam na Pwani. 
Ilielezwa kuwa wananchi wanaoshi katika kijiji hicho kukumbwa na mafuriko kwakuzingirwa na maji hivyo kuhatarisha usalama wa maisha yao, ambapo serikali ilifanya juhudi ya kuwaokoa na kuwahamishia katika sehemu salama.
Hata hivyo zoezi la viongozi hao kufika katika kijiji hicho kilichokubwa na mafuriko hazikuzaa matunda baada ya maji kujaa na kuharibu barabara na hivyo kushindwa kufika katika eneo la tukio.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post