UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA: LEMA KUTOA OFA YA MAGARI ZAIDI YA MATANO


Mbunge wa Arusha Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, ametoa ofa ya magari 10 yatakayotumika kupigia matangazo ya hamasa kwa wananchi, kujitokeza kushiriki vyema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akizungumza leo Oktoba 12, 2019 na EATV & EA Radio Digital, Lema amesema kuwa ameamua kutoa ofa hiyo baada ya kuona magari yanayofanya shughuli hiyo kuwa ni machache na kwamba yupo tayari yawekwe bendera za Chama cha Mapinduzi (CCM).

”Nimewaomba niwape ofa ya magari matano mpaka kumi, watangazie wananchi kwenda kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa, wananchi hawajui na gari ni chache, kwahiyo kama wanahisi kutangazia huko kunaweza kukasababisha wafuasi wengi wa CHADEMA, wakapata ‘awareness’ nimewaomba hayo magari yawekwe bendera za CCM lakini niyalipie mimi” amesema Lema.

Kwa mujibu wa EATV, Hatua hii ya Lema kutoa ofa hiyo ni baada ya yeye kupokea barua kutoka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya, iliyomzuia kufanya mikutano yake ya hadhara jimboni kwake, ambapo hapo siku ya jana Oktoba 11, 2019, aliruhusiwa kuendelea na mikutano yake kama kawaida.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post