TAREHE YA ZOEZI LA UCHUKUAJI NA UREJESHAJI FORM UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA YATANGAZWA

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitangaza tarehe ya uchukuaji na urejreshaji form za kugombea nafasi mbalimbali uchaguzi Serikali za MitaaNa.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, ametangaza rasmi kuanza kwa zoezi la kuchukua na kurejesha form za kugombea nafasi mbalimbali katika ngazi za vijiji, Mitaa, Vitongoji na wajumbe, kwa ajili ya uchaguzi serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake, Jijini Dodoma, Waziri Jafo amesema zoezi hilo litaanza kesho tarehe 29, Octoba na litahitimishwa tarehe 4 Novemba, 2019, zoezi ambalo litakuwa la siku tisa.

Aidha amesema wenye sifa ya kuchukua form ni wale wanaotoka katika vyama vyenye usajili wa kudumu, na kuwataka wale wenye nia ya kuongoza katika serikali za Mitaa ndio mda mwafaka kwenda kuchukua form za kugombea kupitia vyama vyao.

“Zoezi hili litaanza rasmi kesho tarehe 29/10 na litahitimishwa siku ya tarehe 4/11, 2019, na watakao takiwa kugombea ni wale wanaotoka katika vyama vyenye usajili wa kudumu hapa nchini na wale wenye sifa wajitokeze kwa wingi” amesema Waziri Jafo.

Aidha amesema maandalizi yote kwa ajili ya zoezi hilo yamekamilika, na kuwataka watu wote wazingatie kanuni na taratibu wakati wa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa form hizo na kuwataka wasimamizi na wasaidizi wao kusimamia kikamilifu zoezi hilo.

Katika hatua nyingine amewataka Wakuu wa mikoa na Wilaya ambao ndio wasimamizi wa ulinzi na usalama kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama unakuwepo katika mda wote wa zoezi hilo.

Amebainisha kuwa ameshatoa barua ya ufafanuzi  kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kuhusu namna ya uchukuaji na urejeshaji wa form, na amevitaka vyama vyote vizingatie demokrasia wakati wote wa zoezi hilo.

Pia amesema mnamo Oktoba 22, mwaka huu alitoa maelekezo kuwa viongozi wa vijiji, vitongoji, Mitaa, na wajumbe wote uongozi wao ulikoma tarehe hiyo na kwamba shughuri zote zinazohusu ngazi hizo zitafanywa na watendaji wa vijiji, Kata na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Amesema “kuanzia tarehe hiyo wenyeviti wa Mitaa,vijiji, vitongoji na wajumbe, hawataruhusiwa kutekeleza majukumu yao yoyote kwenye maeneo yao, badala yake Kama kutakuwa na Jambo wanapaswa kushirikiana na kuamuliwa na mtendaji wa Kijiji, Kata na Mkurugenzi wa Halmashauri” amesema

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post