SIMBA YAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI MWA MSIMAMO WA LIGI

wachezaji wa timu ya simba wakifurahia goli dhidi ya Singida United leo katika uwanja wa kumbukumbu ya marehemu Shekh Amri Abeid Jijini Arusha

Na.Mwaandishi wetu,Arusha

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Simba wameendelea kukusanya alama tatu baada ya kuichapa  bao 1-0 Singida United leo kwenye Uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Simba huu ni mchezo wao wa Sita wakicheza bila kupoteza hata mechi moja wakifikisha jumla ya alama 18 na kuendelea kukalia usukani wa Ligi hiyo.

Simba walipata bao na la ushindi kwao kupitia kwa Mshambuliaji Kinda  Miraji Athuman “Sheva’ mnamo dakika ya 41 kipindi cha kwanza.

Baada ya mechi hiyo kikosi cha Simba kinatarajia kesho kusafiri kuelekea mkoani Shinyanga kucheza na Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kambarage mjini humo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post