NAIBU KATIBU MKUU MTEULE ASHIRIKI MAKABIDHIANO YA OFISI YA MAJI MWANZA (MWAUWASA) NA MKURUGENZI MPYA MTEULE

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (aliyekaa kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Leonard Msenyele (kushoto) wakisaini nyaraka za makabidhiano ya Ofisi. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji MWAUWASA. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati kulia) akimkabidhi nyaraka za makabidhiano ya Ofisi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (kushoto). Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi MWAUWASA, Christopher Gachuma (wa pili kushoto) na Makamu wake, Edith Mudogo (wa kwanza kulia
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) mara baada ya kumkabidhi Ofisi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA na Mhandisi Msenyele alikuwa Meneja Miradi MWAUWASA. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Gachuma (nyuma katikati) na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi MWAUWASA mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na wafanyakazi wa MWAUWASA (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi Ofisi. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Gachuma (katikati) na Wajumbe wa Bodi ya MWAUWASA.
Baadhi ya wafanyakazi wa MWAUWASA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukabidhi Ofisi. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji MWAUWASA.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post