MWALIMU KATILI ALIYEMVUNJA MGONGO HOSEA APANDISHWA KIZIMBANI

Mahakama ya Wilaya ya Njombe
Na Mwandishi Wetu, APC BLOG NJOMBE

Mwalimu Focus mbilinyi amefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Njombe akikabiliwa na Tuhuma za kumsababishia ulemavu mwanafunzi Hosea Manga anae daiwa kupigwa hadi kuvunjwa mgongo.

Shauri hilo namba 141 la mwaka 2019 linamkabili mwalimu huyo dhidi ya jamhuri kwa kumpiga mwanafunzi hadi kusababishia ulemavu.

Akisoma shauri hilo mwendesha mashtaka wa serikali Elizabeth Malya amesema mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo siku ya marchi 21, 2017  katika  shule ya msingi Madeke kwa kumning’iniza mtoto Hosea Manga dirishani kwa mtindo wa miguu juu huku kichwa kikielekezwa chini na baadae adhabu ya viboko kumi hali iliyompelekea kuanguka chini na kuvunjika mgongo.

Mwendesha mashtaka ameeleza kuwa mwalimu Mbilinyi aliitoa adhabu hiyo baada ya mtoto huyo kufeli maswali ya hesabu kumi alizozitoa darasani .

Hosea ni miongoni mwa wanafunzi sita wanaotajwa kuandibiwa siku hiyo na huku idadi ya viboko ikienda sambamba na idadi ya hesabu walizokosa ambapo yeye alipatiwa adhabu hiyo baada ya kukosa hesabu zote kumi.

Mara baada ya adhabu alipelekwa zahanati ya kijiji cha madeke na ambako madaktari walishindwa kumsaidia  na kuagiza akimbizwe kituo cha afya lupembe ambako nako ilishindikana na baadae akafikishwa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe kibena, kisha Hospitali ya ikonda ambako baada ya kupimwa pia alipewa rufaa ya kupelekwa hospitali ya Taifa ya muhimbili ambapo baada ya vipimo alibainika kuvunjika mgongo.

Mnamo tarehe 4 mwezi april mwaka 2017 mtoto hosea aliruhusiwa kutoka Hospitali ya taifa ya Muhimbili na kupewa baiskeli itakayomsaidia kutembea kutokan na kupooza kwa eneo lote la mwili kuanzia maeneo ya kiunoni hadi miguuni.

Hosea Manga alikumbwa na maswahibu hayo akiwa darasa la tatu mwaka 2017 ambapo hadi sasa alitakiwa kuwa darasa la tano akijiandaa kuingia darasa la sita, lakini hawezi tena kuendelea na masomo kwa sasa kutokana na kuhitaji uangalizi wa karibu akiwa na wazazi wake hususani suala la usafi , kutoka na baadhi ya viungo vyake vya mwili kushindwa kufanya kazi.

Hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Njombe Irvan Msaki ameahirisha kesi hiyo na kutangaza kusikiliza tena nov 12 kutokana na kutokuwako kwa  mashahidi wa upande wa mshtakiwa.

  Mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana .

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post