KIFO CHA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MTOA MACHOZI MBUNGE ELIBARIKI KINGU

 Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu, akilia wakati wa dua ya kumuombea Mzee Jumanne Njoghomi aliyefariki Oktoba 22 mwaka huu nyumbani kwake Kata ya Sepuka mkoani Singida.

 Wakina mama wakiwa kwenye dua hiyo.
 Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu (katikati) akishiriki dua hiyo.
 Katibu wa Msikiti Mkuu Kata ya Sepuka, Juma Mwango akizungumza kwa huzuni.
 Mmoja wa wanafamilia ya marehemu, Ahmed Shabani akilia kabla ya kuanza kwa dua hiyo.
 Vijana wakilia.
 Ni  vilio.
 Ni huzuni tu
 Wazee wakiwa na huzuni wakati wa dua hiyo
 Mwalimu wa Msikiti wa Mtunduruni mjini Singida, Hamisi Ndida akizungumza.
 Wakina mama wakiwa kwenye dua hiyo.
 Ni huzuni tupu.
 Diwani Mstaafu wa Kata hiyo, Juma Ntandu akizungumza.
 Vijana wakiwa wamebeba chakula kwa ajili ya dua hiyo.
Waombolezaji wakiwa kwenye dua ya kumuombea Mzee Jumanne Njoghomi aliyefariki Oktoba 22 nyumbani kwake Kata ya Sepuka mkoani Singida. Marehemu enzi za uhai wake alikuwa ni  aliwahi kuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha Musini Magharibi kwa miaka 15 na mwenyekiti wa Kijiji cha Musini miaka 15.
 
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
KIFO cha Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji Cha Musini na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Sepuka Mkoani Singida,  Mzee Jumanne Njoghomi kimeleta simanzi kubwa kwa watu waliokuwa wakimfahamu na kumtoa machozi Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu wakati wa kumuombea dua marehemu.
 
Wengine walioshindwa kujizuia na kuanza kulia kufuatia kifo cha mwenyekiti huyo ni pamoja na wazee,vijana,wanawake na hali hiyo imetokana na uchapaji kazi, ukarimu na upendo aliokuwa nao kiongozi huyo kwa wananchi.
 
Mbunge Kingu akimuongelea marehemu katika dua hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki alisema kifo chake kimewagusa watu wengi pamoja na yeye kwani alikuwa ni mshauri wake kwa mambo mengi.
 
“Huyu mzee kwangu alikuwa ni baba na mshauri wangu kwa kweli nimepata pigo sana nashindwa namna ya kumzungumzia” alisema Kingu huku akitokwa machozi.
 
Mkazi wa kata hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Lissu alisema hakika kila mtu atavuna alichokipanda akiwa hapa duniani kwani mzee Njoghomi alipanda mema na yameonekana baada ya kifo chake hivyo watu tuliopo baki duniani hatuna budi kujichunguza na kubadilika kwa kutenda mema ya kumpendeza mwenyezi mungu.
 
Ahmed Shabani akizungumza katika dua hiyo alisema ni wakati wa kila mtu kubadilika na  kuachana na vitendo vinavyomchukiza mwenyezi mungu kama kugombea ardhi,uchoyo,wizi,dhuluma na kujivuna kutokana na utajiri na kueleza kuwa vyote hivyo tutaviacha hapa duniani.
 
Mwalimu wa Msikiti wa Mtunduruni uliopo Singida mjini, Hamis Ndiba alisema alichopanda marehemu enzi za uhai wake ndicho kinachojidhihirisha baada ya kifo chake kwani alikuwa mnyenyekevu kwa watu wote na msuluhishi wa migogoro mbalimbali katika mkoa huo.
 
” Marehemu enzi za uhai wake hakumbagua mtu awe mkristo au muislam aliwasikiliza na kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kuwajulia hali wagonjwa na kuhudhuria misibani hakika tumempoteza mtu ambaye alikuwa muhimu sana kwetu” alisema Ndiba.
 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Sepuka, Juma Mghenyi alisema marehemu enzi za uhai wake aliwahi kuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha Musini Magharibi kwa miaka 15 na mwenyekiti wa Kijiji cha Musini miaka 15 na mpaka anafikwa na mauti alikuwa ni mjumbe wa kamati ya siasa wa kata hiyo..

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post