DKT.BASHIRU AMEKUTANA NA UONGOZI WA TGNP NA KUFANYA MAZUNGUMZOKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, leo tarehe 28 Oktoba, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Mtandao wa Wanawake na Katiba na Women Fund Tanzania (WFP).
Katika mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa mtandao wa TGNP kwa niaba ya mashirika mengine Bi. Asseny A. Muro amemkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Katibu Mkuu akipokea mapendekezo hayo ya Ilani, ameyasisitiza mashirika mbalimbali yasio ya kiserikali yaendelee kujikita zaidi kuhamasisha wanawake kwenye sekta za maendeleo ili kuonesha mfano na kuaminiwa zaidi.
Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu Lumumba Jijini Dar es salaam.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post