RC MAKONDA APAMBANA KUTIMIZA MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI


Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Rais Magufuli, kutoridhishwa na utekelezwaji wa baadhi ya miradi ya Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwemo machinjio ya Vingunguti, Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda amelazimika  kushiriki katika ujenzi wa machinjio hayo hadi nyakati za usiku ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika.


Usiku wa kuamkia leo Septemba 22,2019 RC Makonda  aliamua kwenda 'site' usiku kushirikiana na Makandarasi waliopewa tenda ya ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa, ambapo amesema sauti ya Rais Magufuli kuhusu ujenzi huo, imekuwa ikimfuata mara kwa mara hivyo ameona si vyema kumuangusha.

"Nimeamua kusimamia mwenyewe sababu moja tu niliowaamini nakuwaachia kazi hii wameniangusha na ile sauti ya Rais Magufuli, kuwa nimekubali hii miradi ishindikane, isitekelezeke?, nakuambia Rais na Watanzania wote miradi hii ntaisimamia mwenyewe usiku na mchana ili kuhakikisha ndoto uliyonayo katika mkoa wetu inatimia, sitakuangusha" amesema Makonda.

Makonda amesema kwa sasa hatokuwa akipatikana ofisini, badala yake atakuwa akipatikana 'site' hadi miradi hiyo itakapokamilika.

Machinjio hayo yanatarajiwa kukamilika katika kipindi cha ya miezi 3 ijayo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post