RAIS MAGUFULI KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA WAKUU WA POLISI MASHARIKI MWA AFRIKA

Na Woinde Shizza,Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21  wa  Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika Septemba 19 mwaka huu.
Katika Mkutano huo ulioanza septemba 15 kwa wakuu wa vitengo mbalimbali vya polisi kukutana Arusha, Msemaji wa Jeshi la Polisi (SACP)David Misime amesema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika.

Alisema kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo kutatanguliwa na vikao mbalimbali vya wakuu wa vitengo vya Interpol na Septemba 16/17 kutakuwa na mkutano wa wakurugenzi wa upelelezi (DCI)kutoka nchini 14 pia kutakuwa na kikao cha kamati ndogo cha wataalam wa mafunzo  , wataalamu wa sheria na kikao cha wa kujadili unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kikao cha Kuzuia na Kupambana na ugaidi

Alisema kauli mbiu kuimarisha ushirikiano na ubunifu katika kupambana na uhalifu unaovuka mipaka ikiwemo makosa ya kimtandao,ugaidi"

Alisema maandalizi ya mkutano huo yapo vizuri chini ya msimamizi wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na jana wamekaa na wataalamu wa Interpol kutoka Kenya ambao wamefanya kikao

Pia watawapeleka wageni wa mkutano huo chuo cha Polisi Moshi kwaajili ya kuona madarasa mapya na majengo ya hosteli lengo ni kuongeza wanafunzi wengi zaidi kutoka nchi mbalimbali

Pia watawapeleka Gereza la Karanga lililopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kujionea utengenezaji wa viatu vinavyotumiwa na majeshi mbalimbali huku wengine wakuu wa Majeshi ya Polisi  wakienda kutembelewa Hifadhi ya Ngorongoro kujionea Utalii uliopo Nchini

Alisema Septemba 20 kutakuwa na kikao cha mawaziri wa mambo ya ndani kutoka nchi hizo na alitoa rai kwa watanzania kuimarisha amani na utulivu 

Mada zitakazojadiliwa ni kuongeza ushirikiano kwa uhalifu unaovuka mipaka ikiwemo mikakati ya kutoa mafunzo kwa askari wao kwani hivi sasa Sayansi na teknolojia imekuwa pamoja na kuangalia maazimio waliyoyatekeleza katika kikao kilichofanyika mwaka jana nchini Sudani huku Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)Sirro akikabidhiwa rasmi uenuenyekiti mkutanor huo

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post