Rais Magufuli Atangaza Kuwasamehe January Makamba na William Ngeleja kwa kumtukana kwenye simu

Rais Magufuli amesema amewasamehe Mbunge wa Bumbuli, January Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kwa kumtukana kwenye simu.

Akizungumza leo na wataalamu wa ujenzi nchini, Rais Magufuli amesema sauti hizo kwa zaidi ya asilimia 100  zilikuwa za kweli na alipofikilia kama suala hilo litakwenda katika kamati ya maadili ya CCM  hali ingekuwa mbaya kwao.

“Nakumbuka hivi karibuni kuna watu walinitukana na nikapata uhakika kwamba sauti zile ni zao, nikafikiria nikasema hawa wakipelekwa kwenye kamati ya siasa adhabu itakuwa kubwa. Walinitukana kwenye simu na nikahakikisha ni kweli ni sauti zao lakini nimewasmaehe

“Lakini wakajitokeza wawili wakaniomba msamaha nikasema nisipowasamehe nitabaki na maumivu makubwa sana watu hao ni January Makamba na Wiliam Ngeleja nikaona niwasamehe tu.

“Waliomba msamaha nikasema ni vijana  na nimewasamehe. Kama palikuwa na mambo mambo mabaya nyuma tuyasahau ili tukaanze upya maana kusamehe siyo jambo rahisi lakini saa nyingine inabidi usamehe,,” amesema Rais Magufuli. 

Rais Magufuli alikuwa anazungumza katika mkutano wa siku mbili ulioanza leo Dar es Salaam unaohusisha Bodi ya usajili wa Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB),  Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB).

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post