MUFTI ZUBERI AWAFUNDA WATANZANIA, AWATAKA KUZIISHI TABIA ZA MTUME


Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mufti wa Tanzania Sheikh,Abuubakari Zuberi amewataka waislamu na watanzania  nchini kujenga ushirikiano na kusaidiana kwa kuiga tabia za Mtume Muhammad S.W.A kwa kuziishi tabia zake na kuendana na mambo yalio mema na mwisho kufanyakazi kulijenga taifa bila kulalamika wala migogoro.

Mutfi Zuberi ameyasema jijini hapa akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani hapa baada ambapo aliwataka waislamu kuendelea kuidumisha amani ya nchi kwa lengo la kuondoa migogoro baina yao.Amesema kuishi kwa vifundo sio maagizo ya uislamu na kuwataka wale wenye vifundo vyao waache na kurudi kwa Mwenyezi Mungu kwa kile alichodai kuwa hakuna anayeijua kesho yake hivyo busara ni kuwa wachamungu kuishi kwa kuvumiliana na subra ndio muongozo.

Amesema kuwa maisha ya waislamu yawe ni sehemu ya kiigizo chema kwa wengine kwa kuiga tabia za mtume Muhammad s.w.a kama alivyofanya kwa watu wa twaifu, kwa kutanguliza umma mbele badala ya kuwa sehemu ya kuangamiza.

“Busara kwenu sio migogoro ambayo imekuwa ikirudisha shughuli za maendeleo nyuma wala tusiwe watu wa kulalamika kila mara tuchape kazi kwa kujiletea maendeleo na kufanya ibadat hilo ndio lengo la uislamu na hiyo ndio jihad”amesema Mufti Zuberi.

Kwa mujibu wa Mufti Zuberi niwaombe waislamu wote nchi nzima tuishi kwa kupendana na kuheshimiana kwa minajili ya kutaka radhi za Allah na kuwatendea wema wenzetu iwe ni kiigizo chema kuwavuta kwenye dini.

Aidha amewataka kuondokana na mitazamo yenye chuki baina yao na kuijenga jamii yenye ustaarabu kwani uislamu unajengwa na mambo mawili makubwa kujitoa na kujitolea katika dini na maisha yao hivyo waishi kwa kufuata misingi ya dini kwa kuwa tuna kitabu kitukufu Quraan turudi huo pindi tunapohitilafiana.

Akatanabaisha kuwa amani ndio nguzo ya kuabudu kwa misingi ya kuijenga amani nchini kwani bila amani ibada yenye kutulia haipo kwa kuwa uislamu ulifika hadi Hispania lakini walipopiasha waliharibu kila kitu hadi bahari ikawa nyekundu kutokana na wino wa vitabu hivyo busara ndio iwe nguzo ya kuondoa changamoto naina yao.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post