Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya Aamuru Viongozi Wanne wa CHADEMA Wakamatwe

Mkuu wa wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya ameagiza viongozi wanne wa CHADEMA mkoani Kilimanjaro akiwemo Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Lucy Owenya kukamatwa baada ya kutembelea shule ya Sekondari Rundugai wilayani humo kwa madai ya kufanya siasa kinyume cha utaratibu.

Wengine waliokamatwa ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai, Helga Mchomvu, Katibu wa Mbunge wa Hai, Irene Lema na Diwani wa Machame kaskazini, Clement Kwayu.

Sabaya amesema kuwa viongozi hao walikwenda katika shule hiyo leo Ijumaa asubuhi kwa madai ya kuzungumza na wanafunzi na kutoa misaada, bila mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa na taarifa.


Amesema, kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na Serikali,yeyote anayetaka kutoa misaada katika shule yeyote atoe taarifa kwa mkurugenzi wa Halmashauri ili misaada hiyo ijulikane lengo lake na iweze kuratibiwa

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post