Mechi za ligi ya Mabingwa Ulaya-Madrid yaonja muziki wa PSG, Bayern yapeta

Ligi ya mabingwa Ulaya imeendelea jana kwa michezo kadhaa katika viwanja tofauti, kundi A, Paris Saint Germain imewapiga bila huruma Real Madrid goli 3-0, huku Galatasaray ikilazimishwa sare na Club Bruggle.

Kundi B imezikutanisha Olympiacos iliyomaliza kwa sare ya 2-2 na Tottenham Hotspurs, huku Bayern M√ľnchen ikiilaza FK Crvena Zvezda goli 3-0. 

Na katika kundi C, Dinamo Zagreb imeifurumishia mvua ya magoli 4-0 Atlanta, nayo Shakhtar Donetsk imekubali kichapo cha goli 3-0 toka kwa Manchester City. 

Michezo ya mwisho ilikuwa ni kundi D, Atletico Madrid imetoshana nguvu ya goli 2-2 na bibi kizee wa Turin Juventus, nao Lokomotiv Moscow ikiimaliza Bayer Leverkusen kwa goli 2-1.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post