Manchester City yaicharaza Watford 8-0 bila huruma

 Manchester City yailaza watford goli 8-0

Manchester City imefunga magoli matano katika dakika 18 za kipindi cha kwanza huku Bernbard Silva akijipatia hat-trick ya kwanza huku wenyeji hao wakiirarua Watford katika uwanja wa Etihad.

Kikosi cha Pep Guardiola kilifunga katika dakika ya kwanza kupitia David Silva kabla ya Sergio Aguero kuongeza penalti naye Riyad Mahrez akifung bao la tatu.

Bernarndo Silva alifunga bao la nne kupitia kichwa huku Nicholas Otomendi akifunga bao la tano.
Baada ya kipindi cha kwanza kukamilika City iliimarisha mashambulizi yake lakini Bernard Silva alifunga magoli mawili zaidi huku naye Kevin de Bruyne akifunga goli la nane.

Bernardo Silva alifunga hat-trick huku kikosi hicho cha Pep Guradiola kikijipatia ushindi wao mkubwa zaidi tangu alipochokua hatamu 2016.

Pia waligonga mwamba wa goli mara mbili na kuendelea kutafuta magoli mengine hadi mwisho lakini walishindwa kuvunja rekodi ya magoli mengi zaidi katika mechi moja.

Ushindi wa Manchester United wa magoli 9-0 dhidi ya Ipswich mwaka 1995 unasalia kuwa ushindi mkubwa zaidi katika ligi ya Premia na City sasa inaorodheshwa kuwa timu ya saba kushinda mechi kubwa kwa jumla ya magoli manane katika miaka ya hivi sasa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post