MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KUAGA MWILI WA MZEE MUGABE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Keneth Kaunda na Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olubagan Obasanjo wakiteremka kwenye Jukwaa baada ya kutowa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe katika Uwanja wa Taifa wa Michezo jijini Harare Zimbabwe. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Kenya Mhe. Uhuru Kenyata walipokutana wakati wa Hafla ya kutowa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe katika Uwanja wa Taifa wa Michezo jijini Harare Zimbabwe. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro baada ya kutowa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe katika Uwanja wa Taifa wa Michezo jijini Harare Zimbabwe. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Ethiopya walipokutana wakati wa Hafla ya kutowa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe katika Uwanja wa Taifa wa Michezo jijini Harare Zimbabwe. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Hafla hiyo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Nchi za Afrika kwa kushirikiana na Nchi Rafiki Zimeshiriki kwa kiwango Kikubwa Sana katika shuhuli ya kumsindikiza na kumuaga Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe.

Makamu wa Rais Mhe. Samia ameyasema hayo leo wakati wa Shuhuli ya kuaga Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Mugabe iliyofanyika kitaifa katika Uwanja wa Taifa wa Michezo Jijini Harare Nchini Zimbabwe.

Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shuhuli hiyo ambapo alitoa Salamu za Rais kwa Wananchi na Taifa la Zimbabwe. amesema Hotuba ya Rais wa Afrika ya Kusini Sir Ramaphoser aliyoitowa kwa Wananchi wa Zimbabwe na Afrika kwa Ujumla ni kitendo cha Ungwana kwa kuweza kuomba samahani kutokana na Vitendo vinavyoendelea kufanywa wa Wananchi wa Afrika ya kusini.

Nae Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afirka Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro amesema Marehemu Mzee Mugabe ni kipenzi cha Wananchi wa Zimbabwe na Waafrika kwa Ujumla hivyo hakuna budi kumuenzi na kuyaendekleza yale yote mazuri aliyo yaacha.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post